January 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Chadema yataka NEC iongeze BVR

Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Zanzibar, Salum Mwalim

Spread the love

NAIBU Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Zanzibar, Salum Mwalim, ameitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kuongeza mashine za BVR ili kuongeza kasi ya uandikishaji katika daftari la kudumu la mpiga kura. Anaandika Moses Mseti, Mwanza … (endelea).

Mwalimu ametoa kauli hiyo katika ziara yake ya ukaguzi wa uandikishaji katika wilaya mbili za Nyamagana na Ilemela mkoani mwanza jana.

Amesema NEC inao wajibu wa kusimamia kazi hiyo inafanyika kwa muda muafaka ili kuwapa fursa wananchi kumchagua kiongozi anayefaa katika kuwatumikia.

Mwalimu amesema endapo NEC haitawaandikisha wananchi wote, Chadema itawashawishi kuandamana ili kuongezewa kwa muda wa uandikishaji.

Hata hivyo, amesema kitendo cha Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuandikisha wafuasi wao ni dhahiri kinaonesha anguko lao limefika kutokana na mbinu chafu wanazozifanya.

“Kama mlivyojionea wenyewe leo hapa tumemkuta Afisa Mtendaji mmoja anaandikisha watu kinyume na utaratibu, yeye anachopaswa kukifanya ni kuhamasisha watu kujiandikisha.

“Hizo zote ni mbinu zao chafu, hatuwezi kuandikisha watu ambao wanadhani ni wafuasi wao na wengine wanaendelea kupanga msitari,” amesema Mwalimu.

Pia, amesema NEC inapaswa kuongeza vifaa ili kuendana na idadi ya watu waliopo katika mkoa husika ili kuongeza kasi ya uandikishaji na kutatua kero zinazoweza kujitokeza.

Kwa mujibu wa Mwalimu, endapo vifaa vitaongezwa hata muda wa uandikishaji nchi utakuwa mfupi kutokana na wingi wa vifaa, jambo ambalo litafanikisha uchaguzi kufanyika kwa mujibu wa kanuni na utaratibu.

Wakala wa Chadema katika Kata ya Igombe, Peter Mweya, amesema uandikishaji kwenye eneo hilo unafanyika kwa amani lakini mashine zilizopo hazitosherezi na wakati mwingine hupata hitirafu.

Amesema idadi ya watu wanaoandikishwa iliyotolewa na NEC kwamba mashine majo inaweza kuandikisha watu 160 kwa siku kama mwandikishaji atakuwa na kasi, mambo bado ni tofauti kwani kwa siku wanaandikishwa 80.

“NEC ilivyosema sio kweli hata kama mwandikishaji atatumia dakika tatu ama tano, hao watu hawawezi kufika, siku nne hata watu 500 hawatafika,” amesema Mweya.

error: Content is protected !!