Wednesday , 27 September 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Chadema yasisitiza kufanya maandamano kesho
Habari za SiasaTangulizi

Chadema yasisitiza kufanya maandamano kesho

Patrobass Katambi, Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Chadema Taifa (BAVICHA). Picha ndogo IGP Simon Sirro
Spread the love

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesisitiza kwamba maandamano ya amani ambayo yalipangwa kufanyika kesho nchi nzima yatafanyika, anaandika Hellen Sisya.

Akizungumza na MwanaHalisi Online, Edward Simbeye, katibu mwenezi wa Baraza la Vijana la chama hicho (Bavicha), amesisitiza kuwa maandalizi kwa ajili ya maandamano hayo yanaendelea vizuri na tayari chama hicho kilishaandika barua kulitaarifu jeshi la polisi kuhusiana na uwepo wa maandamano hayo katika kila mkoa nchini.

Aidha, kiongozi huyo amesema kuwa mpaka muda huu bado jeshi hilo halijajibu barua ambayo chama hicho kimeliandikia na kuongeza kuwa maandamano hayo yatafanyika hata kama jeshi hilo litakuwa halijajibu barua yao mpaka kufikia siku ya kesho.

“Maandalizi yanaendelea vizuri na hapo kesho tutatoa muongozo kwa wanachama wetu na wananchi kwa ujumla kuhusiana na mahali ambapo maandamano hayo yataanzia na kuishia katika kila mkoa nchini.” amesema Simbeye

Akifafanua kuhusiana na tabia ya jeshi la polisi kuzuia kufanyika kwa maandamano kwa sababu mbalimbali, Simbeye amesema kuwa maandamano ni haki ya kikatiba na jeshi la polisi lina wajibu wa kulinda wananchi ambao wanatumia haki yao ya kikatiba kufanya maandamano na si kuzuia maandamano na kuongeza kuwa maandamano hayo yatafanyika hata kama jeshi hilo litazuia maandamano hayo.

Wiki iliyopita, baraza hilo la vijana lilitangaza kuwepo kwa maandamano ya amani siku ya kesho ambayo waliyapa jina la “Black Thursday” yenye lengo la kushinikiza kuwepo kwa haki za kisiasa, kiuchumi, utawala wa sheria pamoja na haki za binadamu nchini.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga: Usambazaji umeme vijijini mwisho Desemba 2023

Spread the love  NAIBU Waziri wa Nishati, Judith Kapinga, amesema ifikapo mwezi...

Habari za Siasa

Mgongano wa kimasilahi wamhamisha Chande TTTCL

Spread the love  ALIYEKUWA Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO),...

Habari za SiasaTangulizi

Mgawo wa umeme: Rais Samia ampa miezi sita bosi mpya TANESCO

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amempa miezi sita Mkurugenzi...

Habari za Siasa

Rais Samia avunja bodi ya REA

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua Balozi Jacob Kingu, kuwa...

error: Content is protected !!