Sunday , 29 January 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Chadema yasema kikokotoo cha mafao hakina uhalisia wa umri wa kufanya kazi
Habari za Siasa

Chadema yasema kikokotoo cha mafao hakina uhalisia wa umri wa kufanya kazi

Spika wa Bunge la Wananchi la Chadema, Celestine Simba
Spread the love

 

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimekosoa kikokotoo kipya cha mafao na kueleza kuwa kimekosa uhalisia wa umri wa mtu kuanza kazi hadi kustaafu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam …. (endelea).

Chadema imekosoa kikokotoo hicho kupitia kwa Spika wa Bunge la Wananchi la Chadema, Celestine Simba, katika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika leo Jumatatu tarehe 28, Agosti, jijini Dar es Salaam.

Simba amesema mfanyakazi alikuwa anakadiriwa kuwa ameanza kazi akiwa na miaka 15 ili aweze kufanyakazi kwa miaka 45 kabla ya kustaafu akiwa na umri wa miaka 60. “Hapo ndipo wale wanaojiita wataalam wa mambo ya hifadhi za jamii walikuja na kikokotoo cha 1/540,” amesema Simba.

Hata hivyo amesema kwa mfumo wa elimu ambao unamtaka mwanafunzi kuanza darasa la kwanza akiwa na umri wa miaka 7 na asome madarasa ya msingi 7 na aongeze madarasa 4 ya sekondari maana yake tayari anakuwa na miaka 18 na akiongeza mawili ya kidato cha tano na sita tayari anakuwa na miaka 20 akienda chuo miaka 3 tayari ana miaka 23.

“Hapo akipata ajira kwa kikokotoo hicho maana yake atafanya kazi kwa miaka 37 ndio astaafu na hivyo kiuhalali kikokotoo chake kingekuwa 1/444 na sio kwa 540 ambayo ni kwa Yule ambaye anatakiwa kufanyakazi kwa miaka 45.

“Swali la kujiuliza ni kwamba, hawa wataalamu wa hesabu wa mifuko, wameitoa wapi hiyo miezi 580 ambayo sasa ndiyo itatumika kama msingi katika kukokotoa mafao ya mstaafu?,”amehoji Simba.

Amesema kwa muktadha huo ni kuwa ili mtu afanye kazi kwa miaka 48 na kustaafu akiwa na miaka 60 ni lazima mtu huyo aanze kazi akiwa na umri wa miaka 12.

“Kwa mfumo wetu wa elimu hapa Tanzania ni kwa njia gani mtoto anaweza kuanza kazi akiwa na umri huo wa miaka 12?” amehoji

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

NCCR-mageuzi yawaangukia Polisi kupotea kwa kada wake

Spread the loveJESHI la Polisi nchini limeombwa kufanya uchunguzi wa kina utakaosaidia...

Habari za Siasa

Uamuzi kesi ya kupinga Bodi ya Wadhamini NCCR-Mageuzi kutolewa Februari 6

Spread the love  MAHAKAMA Kuu, Masjala Kuu ya Dar es Salaam, imepanga...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu:Suluhu ya ugumu wa maisha ni Katiba Mpya

Spread the love  MAKAMU mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo-Chadema Bara,...

Habari za Siasa

Lissu: Miaka 30 ya vyama vingi haikupambwa kwa marumaru

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo-Chadema, Tundu...

error: Content is protected !!