July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Chadema yaongeza muda uchukuaji fomu

Kutoka kushoto, Afisa Habari wa Chadema, Tumaini Makene, Naibu Katibu Mkuu, John Mnyika na Mohamed Mtoi

Spread the love

CHAMA cha Demokrasia na maendeleo (Chadema), kimefungua rasmi milango kwa watu wenye nia na sifa za kuwania ubunge na udiwani katika majimbo yenye wabunge wa chama hicho. Anaandika Sarafina Lidwino … (endelea).

Aidha, hatua hiyo imekuja baada ya   Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kutangaza majimbo mapya 26 ya uchaguzi, ambamo  Chadema   kimelazimika kupangua ratiba ya awali na kutoa ruhusa kwa wanachama wote wenye sifa  ya kuchukua fomu za uteuzi ndani ya majimbo hayo mapya kwa nchi nzima.

 Katibu Mkuu CHADEMA, Dk. Willibroad Slaa, amesema, kuwa wananchi wote wenye nia na sifa za kuchukua fomu za ubunge kwenye majimbo yote yakiwemo mapya wanaruhusiwa kufanya hivyo kuanzia Julai 15 hadi 19 mwaka huu, kuazia sa 10 jioni.

Kwa mujibu wa Silaa, kwa nafasi za udiwani zoezi la kuchukua fomu na kurejesha fomu katika kata zote nchini limeongezwa muda ambapo litafanyika kuanzia Julai 15 hadi 29 mwaka huu.

 Itakumbukwa kuwa hapo awali CHADEMA ilitoa ratiba yake ya uteuzi wa ndani ambapo ilionesha kuwa uchukuaji na urejeshaji wa fomu za kuwania udiwani na ubunge katika kata na majimbo yenye madiwani au wabunge wa chama hicho ulitakiwa kusubiri hadi halmashauri zitakapokoma au bunge litakapokuwa limevunjwa.

Pia amesema kutokana na kuongezwa kwa majimbo hayo 26, kwa upande wa Tanganyika, fomu za kuwania uteuzi katika majimbo hayo zitaendelea kutolewa katika ngazi ya taifa, mkoa, wilaya na jimbo kwa utaratibu ule ule ambapo makatibu wa majimbo mama (yale ya zamani) wataendelea kutoa fomu kwa ajili ya majimbo mapya.

“Wagombea ambao walishachukua na kurejesha fomu wana haki ya kuamua jimbo lipi wanaenda kugombea na hawalazimiki kuchukua fomu upya…watatakiwa kuujulisha uongozi wa chama ngazi ya jimbo kwa barua rasmi kuonesha kuwa fomu yake iwe ni ya jimbo lipi kati ya jimbo mama ama jipya na nakala ya barua hiyo inakiliwe ngazi ya wilaya, mkoa, kanda na taifa,” ameelekeza  Slaa.

Mbali na hilo,  amezungumzia kuhusu suala la kura ya maoni kwa upande wa wabunge na kusema, amewaagiza waratibu wa kanda, wenyeviti na makatibu wa jimbo  ya kwamba, majimbo yote yanatakiwa kuanza zoezi la kura ya maoni Julai 20 hadi 25 mwaka huu, kwa kuzingatia taratibu ya kura ya maoni.

“Kwa majimbo  yaliyogawanywa kila jimbo litafanya mchakato wake wa kura ya maoni kwa kusimamiwa na mamlaka zilizotajwa katika miongozo husika ya maoni ambapo  litafanyika kwa siku 6 mfululizo,” amesema Slaa.

Hata hivyo, amesisitiza kuwa, kanda inapaswa kuweka ratiba yake ya ndani katika muda huo na kuhakikisha kuwa majimbo yote, ya zamani na mapya, katika kanda husika yakamilishe kura za maoni ndani ya tarehe hizo.

Amebainisha,“Kamati Kuu iliazimia pia kuwa kura za maoni nafasi ya udiwani zitaanza kufanyika kuanzia tarehe 30 Julai hadi 5 Agosti, 2015. Hii maana yake ni kuwa zoezi la kura za maoni kwa nafasi ya udiwani litaanza baada ya kumalizika kwa zoezi la kura za maoni nafasi ya ubunge,” amesema Slaa.

error: Content is protected !!