Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Chadema yaomba miaka mitano kuiongoza Tanzania “tutawaondoa kwenye umasikini”
Habari za Siasa

Chadema yaomba miaka mitano kuiongoza Tanzania “tutawaondoa kwenye umasikini”

Wanafunzi wa shule ya msingi wakiwa wamekaa chini baada ya kukosa madawati
Spread the love

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimewaomba Watanzania wakipe ridhaa ya kuiongoza nchi kupitia sanduku la kura, kwani kitawaondoa katika umasikini ndani ya miaka mitano. Anaripoti Mwandishi Wetu, Njombe … (endelea).

Ahadi hiyo imetolewa leo tarehe 27 Februari 2023, mkoani Njombe, katika mkutano wa hadhara wa Chadema, ambapo mgeni rasmi alikuwa Mwenyekiti wa chama hicho taifa, Freeman Mbowe.

Akizungumza katika mkutano huo, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, John Heche, amedai kwamba umasikini wa Tanzania niwakutengeneza, kwa kuwa wananchi wamekipa dhamana ya uongozi chama ambacho hakina uwezo wa kuleta mabadiliko.

Mwanasiasa huyo ameonesha kushangazwa na kitendo cha nchi kuagiza bidhaa nje ya nchi, ambazo zinaweza kuzalishwa nchini kama samani za ndani.

“Umasikini tulio nao niwakutengeneza, leo CCM ingekuwa na akili hapa Njombe kungekuwa na viwanda vikubwa vya samani, samani zinasafirishwa nje ya nchi. Leo tunaagiza mpaka njiti za kutolea nyama kwenye meno kutoka China,” amesema Heche.

Heche amesema “hawa watu wamechoka wanataka kutufanya masikini, sisi hatuhitaji umasikini mkitupa nchi, tupeni miaka mitano tunawaondoa watu wote kwenye umasikini ili kila mtu aishi kwake na aendeshe gari lake. China imetumia miaka 30 kuondoa watu milioni 800 kwenye umasikini.”

John Heche

Mjumbe huyo wa Kamati Kuu Chadema, amekosoa hatua ya Serikali kujenga reli ya kisasa (SGR), kwa kutumia vyuma vinavyotoka nje ya nchi, wakati mkoani Njombe kuna vyuma na makaa ya mawe ambayo kama yangechimbwa yangesaidia kushusha gharama za ujenzi huo.

Naye Mjumbe wa Kamati Kuu Chadema, Ezekiel Wenje, amedai kwamba Watanzania wanakumbatia umaskini kwa kuendelea kuiweka madarakani CCM.

“Wakati mwingine mtu umasikini anataka ajilimbikizie, sababu wewe masikini mtoto wako anaenda shule mbovu, unakunywa maji machafu, umeme unakatika kila siku na unaambiwa sababu CCM wameshindwa kuibadilisha nchi hii, bado unawapigia kura na unawakumbatia,” amesema Wenje.

Mjumbe mwingine wa kamati hiyo ya Chadema, Patrick Ole Sosopi, amedai kwamba CCM haistahili kuongoza nchi kwa kuwa imeshindwa kufanya mageuzi ndani ya miaka 60 iliyokaa madarakani.

“Tunahitaji kusaidiana nchi hii, Watanzania tuungane tuiondoe CCM, haistahili kuiongoza nchi hii hata jana, yaani leo kesho walipaswa kuondoka sababu wameshindwa kutatua shida za watanzania. Naomba muiamini Chadema,” amesema Sosopi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Dk. Mwakyembe : Zanzibar waliongoza kutaka Serikali 2 za muungano

Spread the love  MWANASIASA mkongwe nchini, Dk. Harrison Mwakyembe, amesema mjadala wa...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ataja mikakati ya kufikia trilioni 2 biashara Uturuki, Tz

Spread the loveWakati Tanzania na Uturuki zikidhamiria kuongeza kiwango cha biashara hadi...

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

error: Content is protected !!