July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Chadema yamvaa Bulembo

Spread the love

KAULI ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdallah Bulembo kwamba “CCM haitafanya makosa kukabidhi Ikulu kwa wapinzani” imezua mjadala. Anaandika Faki Sosi … (endelea).

Bulembo alitoa kauli hiyo kwenye mkutano wa kampeni za urais wa mgombea wa chama chake Dk. John Magufuli Kigoma.

“Serikali imefanya makosa mengi na Chama Cha Mapinduzi kimefanya makosa mengi lakini hakitofanya kosa la kuruhusu chama pinzani kuingia Ikulu,” amesema Bulembo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo kwenye Ngome ya UKAWA, Jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amemtaka Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (NEC), Jaji Damian Lubuva kukemea kauli hiyo.

Pamoja na hivyo Mbowe ameitaka CCM kufuta kauli kwa kuwa ni ya uchochezi ambayo inatoa tafisiri ya kutokuwepo umuhimu wa kufanya uchaguzi.

Mbowe amesema kuwa, tangu kutolewa kwa kauli hiyo, hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa na NEC wala kiongozi yoyote wa CCM aliyekemea au kuzungumzia na kuwa “inaonekana ni mipango ya chama hicho.”

Amesema kuwa, kauli hiyo ingetolewa na chama pinzani NEC isingevumilia na ingechukua hatua haraka.

Hata hivyo amesema CCM inalindwa na sheria mbovu na kandamizi na kuwa, zinahitajika kuondolewa.

Amefafanua kuwa, mfano wa sheria hiyo ni kutangazwa kwa matokeo ya urais ambapo kwa mujibu wa sheria hayapingwi mahakamani.

error: Content is protected !!