Thursday , 25 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Chadema yamtaka Dk. Mwigulu ajiuzulu uwaziri
Habari za Siasa

Chadema yamtaka Dk. Mwigulu ajiuzulu uwaziri

Dk. Mwigulu Nchemba, Waziri wa Fedha na Mipango
Spread the love

 

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimemtaka Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba, kujiuzulu wadhifa wake ili kupisha uchunguzi wa tuhuma za malipo ya baadhi ya miradi nje ya bajeti. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Wito huo umetolewa leo tarehe 7 Februari 2023 na Mjumbe wa Bunge la Wananchi la Chadema, Ahobokile Mwaitenda, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

“Mwigulu na wote waliohusiska na malipo nje ya bajeti wapishe uchunguzi huru wa kilichofanyika kwenye matumizi nje ya bajeti bila ruhusa ya bunge na kuvunja sheria mbili za wizara ya fedha,” amedai Mwaikenda.

Mwaikenda ametaja baadhi ya maeneo ambayo amedai fedha zake zilitolewa nje ya bajeti ikiwemo ununuzi wa mbolea uliogharimu Sh. 86 bilioni, pamoja na malipo ya kiasi cha Sh. 350 bilioni yaliyofanywa na Serikali katika Kampuni ya Symbion, kama fidia ya kuvunja mkataba kinyume cha sheria.

Katika hatua nyingine, Mwaikenda amedai kuna ubadhirifu katika mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR), kipande cha kutoka Tabora hadi Kigoma, akidai mkataba wa ujenzi wa kipande hicho ulikiuka sheria za nchi kwa kuwa mkandarasi alipatikana bila ushindani.

“Upatikanaji wa mkandarasi kwa singlesource limit (bila ushindani)zake zikoje ? Imekuaje mradi wa SGR kutoka Tabora –Kigoma iingie mkataba lot 6 wa km 506 , kwa Sh. 6.34 trilion , wakati hapo hapo ilikuwa na mkataba Isaka –Mwanza wa km 341 wa Sh. 3.12 trillion. Gharama za Isaka -Mwanza ni Sh. 9.1 billion wakatii Sh. 12.5 billion kwa kilomita,” amedai Mwaikenda.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

error: Content is protected !!