July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Chadema yalinyosha bunge

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akifurahia jambo Mbunge wa Viti Maalum, Margaret Sitta (katikati ) na Mbunge wa Korogwe, Stephen Ngonyani kwenye viwanja vya

Spread the love

VUTA nikuvute kati ya Bunge na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) imefikia tamati baada ya serikali kuagizwa kutoa ripoti ya usajili na uendeshaji tata wa Chuo Kikuu cha Kampala Kampasi ya Dar es Salaam (KIU) na Chuo cha Mtakatifu Joseph kilichopo Arusha. Anaandika Dany Tibason kutoka Dodoma … (endelea).

Wabunge wa Chadema waliibana serikali wakiitaka itoe ripoti ya sintofahamu inayoendelea kuhusu vyuo hivyo ambapo bunge liliridhia kuwasilishwa taarifa hiyo kwa muda usiopungua wiki moja.

Agizo hilo limetolewa juzi na Mwenyekiti wa Bunge, Lediana Mng’ong’o wakati wa kupitisha Bajeti ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, ikiwa ni baada ya Mbunge wa Viti Maalum, Susan Lyimo (Chadema) kuitaka serikali kuelezea kwanini katika vyuo hivyo kuna migogoro?

Akitoa agizo hilo, Mng’ong’o  alisema, suala hilo ni lazima litolewe majibu kwa kushirikisha Kamati ya Huduma za Jamii, mtoa hoja Susan Lyimo (Chadema) na wizara mtambuka.

Awali, Lyimo wakati bunge lilipokaa kama kamati, alitishia kutoa shilingi kwa kile alichodai kuwa serikali imeshindwa kutatua mgogoro huo ambapo alitoa mfano mgogoro wa KIU kuhusu wanafunzi kusoma masomo ya Famasia na kuhitimu huku wakiwa hawana sifa ya kusoma masomo hayo kulingana na utaratibu wa mfumo wa Elimu ya Tanzania.

Lyimo alisema wanafunzi hao wamesoma masomo ya sanaa (Arts), wakati kiutaratibu walitakiwa wawe wamesoma masomo ya sayansi.

Lyimo alisema kutokana na mgogoro huo wanafunzi ambao walihoji kutokupata usajili kwa msajili wa mfamasia, 16 walifukuzwa.

Kutokana na hoja hiyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma za Jamii, Margareth Sitta, alichangia kwa kuunga mkono hoja ya Lyimo akisema suala hilo lilifika kwenye kamati yao ambapo walimwalika yeye (Lyimo) na walivyolichunguza waligundua kuwepo kwa matatizo mengi katika vyuo hivyo.

Sitta alimuomba Lyimo apokee ombi la Naibu waziri, Anna Kilango, kuhusu serikali kulifanyia kazi suala hilo kwa kuwa  ni zito, hivyo walifanyie kazi ila mwenyekiti atoe agizo kwa serikali lini walete taarifa hiyo.

Akichangia hoja hiyo, Mbunge wa Nyamagana, Ezekia Wenje,

 (Chadema)  alisema, hii ni aibu nyingine tena kwa serikali na kwamba ni sawa na aibu ile ya wagonjwa kupasua kichwa badala ya goti na goti badala ya kichwa.

Wenje amesema, serikali inapaswa kueleza ni kwa namna gani wanafunzi hao waliosoma miaka minne kiwa wakaambiwa hawatambuliwi walichokisoma lakini pia ni vipi namna gani watafidiwa gharama zao.

“Ingekuwa nchi nyingine viongozi wote, Waziri wa Elimu, watumishi wa TCU na hao wenye vyuo wangewajibika kwani ni aibu kwa taifa,” anasema.

Akielezea sakata hilo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Jenister Mhagama alisema, suala hilo limepokelewa na serikali na watalifanyia kazi kwa wakati kwa kuwa ni aibu na haliwezi kukubalika.

Amesema, suala hilo ni mtambuka hivyo ni vyema kuwepo kwa ushirikiano kati ya kamati, wizara husika na taasisi zingine ambazo kwa pamoja zimehusika kuwepo kwenye sakata hilo.

error: Content is protected !!