June 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Chadema yaitikisa CCM Morogoro

Katibu wa Chadema Mkoa wa Morogoro, Samwel Kitwika

Spread the love

WAKATI Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kikiwa katika mchakato wa kutoa fomu kwa wagombea udiwani, ubunge na urais, mkoani Morogoro, watia nia wameanza kuitia hofu CCM. Anaandika Bryceson Mathias … (endelea).

Hivi karibuni, akiwa mkoani Mwanza katika ziara za kuimarisha chama, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, aliwataka wanachama wao wanaotaka kuwania uongozi huo, wajielekeze zaidi katika maeneo ambayo hawana wawakilishi kwa sasa.

Mkoani Morogoro agizo hilo limeanza kutekelezwa kwa kishindo. Akizungumza na MwanaHALISIOnline, Katibu wa Chadema mkoa, Samwel Kitwika amesema, majimbo yote 10 yamevamiwa na watia nia wa Chadema.

Pia, Kitwika amesema kuwa kata 212 za Morogoro, ziko kwenye mtikisiko, ambapo watia nia wanajitokeza kwa wingi kuchukua fomu.

Kitwika alibainisha idadi ya watia nia waliojitokeza hadi sasa na majimbo yao kwenye mabano kuwa ni 11 (Kilombero), 4 (Mikumi), 5 (Kilosa Kati), 3 (Gairo), 4 (Mvomero), na 7 (Manispaa ya Morogoro).

“Morogoro Kusini Mashariki wako watatu, Ulanga Magharibi (7) na Ulanga Mashariki (2) na Ulanga Magharibi tuna asilimia 100 tutashinda,”amesema Kitwika.

error: Content is protected !!