
Suzan Kiwanga
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kwa mara nyingine tena kimekibwaga Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika kesi ya kupinga matokeo ya Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kihonda Maghorofani. Anaandika Bryceson Mathias, Morogoro… (endelea)
Kesi hiyo namba 2/2015 iliyofunguliwa na Waziri Makumlo, aliyekuwa mgombea wa CCM dhidi ya Elizeus Rwegasira wa Chadema, akidai kwamba hakuwa mshindi halali.
Makumulo aliyekuwa akitetewa na wakili Tumaini Mfinanga, alionesha kukata tamaa ya kupata ushindi baada ya kushindwa kufika mahakamani katika kesi ambayo Rwegasira alikuwa akitetewa wakili Barthromeo Tarimo.
Kutokana na mlalamikaji kutohudhuria mara mbili mfululizo, wakili wa mlalamikiwa, aliiomba mahakama iifute kesi hiyo, jambo lililoungwa mkono na mwakilishi wa Manispaa pamoja na wakili wa mlalamikaji.
Hatimaye, Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Morogoro, Agnes Ringo, aliifuta kesi hiyo na kumtangaza Rwegasira (Chadema), kuwa mshindi wa uchaguzi huo wa Desemba 14, 2014.
More Stories
ACT-Wazalendo yasema bei ya vyakula imepaa, yatoa mapendekezo
CCM yataka viingilio Sabasaba vipunguzwe
Mahakama yasema uamuzi kesi ya kina Mdee haujakamilika