Sunday , 25 February 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Chadema yafichua siri nzito kukabiliana na Magufuli
Habari za SiasaTangulizi

Chadema yafichua siri nzito kukabiliana na Magufuli

Frederick Sumaye, Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Pwani (katikati) akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani
Spread the love

HATIMAYE Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimefichua siri nzito kwamba kina program maalum kwa ajili ya kupambana na kandamizaji wa demokrasia unaofanywa na Rais John Magufuli, anaandika Mwandishi wetu.

Siri hiyo imedokezwa kwa MwanaHALISI online leo na Mjumbe wa Kamati Kuu Frederick Sumaye.

Sumaye ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kanda ya Pwani ya Chadema, alisema chama hicho hakijakaa kimya kama inavyoonekana na kwamba ipo program maalum ambayo anaamini itasaidia kupambana na ukandamizaji huu.

”Kama  Rais Magufuli hataki sisi tufanye siasa ni aje ni mapngo maalum wa kufuta mfumo wa vyama vingi hapa nchini,” alisema.

”Lakini ilimradi hathubutu kufuta vyama vya siasa ni lazima tuendelee kufanya siasa,” amesema Sumaye.

Unaweza kumtazama zaidi  kwenye Video hii….

Amesema program hiyo inaratibiwa na chama na kwamba muda siyo mrefu anaamini kwamba wataendelea kufanya siasa hapa nchini.

Ameongeza kuwa licha ya kuwapo  program hiyo ya kukabiliana na matatizo haya ya ukandamizaji wa demokrasia unaofanywa na Rais Magufuli,  lakini pia italenga kukieneza chama kwa Watanzania.

Sumaye ambaye alishika nafasi ya Uwaziri Mkuu kwa miaka 10 mfululizo, amesema hawapo kimya na kwamba pale wanapominywa watahakikisha wapaza sauti zao kwa kusema.

Kuhusu Madiwani wa Chadema kuhamia CCM, Sumaye amesema siasa hizo zimepitwa na wakati na kwamba kinachotakiwa kufanywa na CCM siyo kurubuni viongozi wao na kuwachukua bali kufanya vitu ambavyo vitawavutia Watanzania wakipende.

”Kazi inayotakiwa kufanywa na CCM ni kuimarusha chama hicho na siyo kuchukua madiwani ama viongozi wengine kwa kudhani kwamba ndiyo wanadhoofiha vyama vingine vya upinzani.

Amesema CCM kwa sasa hakifanyi siasa bali kinajivunia dola ambayo inawabeba na kwamba mwaka 2020, lazima kiondoke madarakani.

”Badala ya kutatua matatizo ya wananchi wao wananunua madiwani ili kionekani kina nguvu,” amesema
Kinachofanya  chama kiwe na nguvu ni kutatua matatizo ya watu na kwa sasa watu wanaogopa kusema kwa sababu ya hofu ya dola na siyo kitu kingine.

Kuhusu kudumisha umoja wao wa Ukawa, Sumaye amesema wana mipango mingi ili kuhakikisha wanamsaidia, Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF),  Maalim Seif Shariff  Hamad.

Amesema lengo serikali kumsaidia Ibrahim Lipumba ni kutaka kudhoofisha chama hicho pamoja na Ukawa na kwamba wamegundua hilo na wamejipanga kukabiliana nalo.

Ameongeza kuwa lengo ni kumdhoofisha Maalim Seif kwa sasabu wanajua CCM haiwezi kushinda uchaguzi kwa upande wa Zanzibar.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Samia atoa pole ajali iliyoua 25, kujeruhi 21 Arusha

Spread the loveRais Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za rambirambi kwa Mkuu...

Habari MchanganyikoTangulizi

25 wafariki dunia katika ajali Arusha

Spread the loveWatu 25 wamefariki dunia papo hapo mkoani Arusha katika ajali...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Biteko afuta likizo watumishi Tanesco, bosi Morogoro yamkuta

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dk. Doto...

Habari za Siasa

Mbarala ajitosa kumrithi Zitto, aahidi kuipa ushindi ACT-Wazalendo uchaguzi mkuu

Spread the loveKATIBU wa Idara ya Haki za Binadamu na Makundi Maalum...

error: Content is protected !!