Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Chadema yaanza safari kutafuta uongozi Kinondoni
Habari za Siasa

Chadema yaanza safari kutafuta uongozi Kinondoni

Spread the love

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Jimbo la Kinondoni, Dar es Salaam, kimeanza safari ya kusaka uongozi kata na jimbo hilo, katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020. Anaripoti Regina Mkonde, Kinondoni … (endelea).

Jana Ijumaa tarehe 4 Septemba 2020 wagombea udiwani na ubunge wamezindua rasmi kampeni za uchaguzi huo, katika Uwanja wa Fisi, Tandale jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika mkutano huo, Susan Lyimo, mgombea Ubunge wa Kinondoni kupitia Chadema, alisema ameamua kugombea jimbo hilo ili atatue kero za wananchi hasa ya elimu na afya.

“Tumekuwa washabiki, tunashabikia kusema Serikali imefanya mambo makubwa amenunua ndege, ndege na WanaTandale wapi na wapi?,” alisema Susan ambaye ni mbunge wa viti maalum aliyemaliza muda wake

Susan alisema, wamejipanga kuhakikisha wanaongoza jimbo hilo na nchi kwa ujumla na kuwaomba Watanzania kuwachagua wagombea wa Chadema ili kwenda kuwatumikia kwani Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeshindwa.

Naye Hamad Ramadhani, mgombea udiwani wa Tandale akizungumza katika uzinduzi huo, alisema ameamua kugombea kata hiyo kwa kuwa ilikosa kiongozi sahihi kwa muda mrefu.

“Kwa miaka mingi Tandale imekosa mtu wa kuongoza nikaona nije nigombee. Kuna kero nyingi mfano takataka katika nyumba zetu, awali miaka ya nyuma zilikuwa zinabebwa na halmashauri ya manispaa lakini sasa hivi mzigo wote wameachiwa wenyeviti wa serikali za mitaa.”

“Mkinichagua kuwa diwani wenu, nitakwenda kulisemea suala hili katika baraza la manispaa ili turudi mfumo wa zamani wa kuweka vizimba vya taka,” alisema Ramadhan.

Wakati huo huo, Ramadhan ameahidi kupambana vijana wapate mikopo inayotolewa na halmashauri, endapo atafanikiwa kuwa diwani.

“Endapo mtanichagua nitaingia baraza la madiwani nitaenda kuelekeza namna bora ya ukusanyaji takataka. Nitakwenda kusemea kuhusu suala la mikopo lakini hizi pesa ziko kwa ajili ya vijana endapo mtanichagua nitakwenda kulisemea hili katika halmashauri ya wilaya,” ameahidi Ramadhani.

Kwa upande wake, Waziri Muhuzi, Mwenyekiti Chadema Wilaya ya Kinondoni aliwashauri Watanzania kuchagua viongozi watakaotekeleza sera zao kwa kusikiliza matakwa ya wananchi na sio matakwa yao binafsi.

David Raphael, Katibu wa Chadema Jimbo la Kinondoni aliwaomba Watanzania wamchague Tundu Lissu, mgombea urais wa Tanzania kupitia chama hicho na wagombea ubunge na udiwani wa chama hicho ili awaletee maendeleo.

Naye Benjamin Kambarage, Mwenyekiti Baraza la Vijana Chadema (Bavicha) kata ya Tandale aliwataka vijana kuchagua wagombea wa chama hicho, kwa maelezo kwamba kitaheshimu haki zao.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

error: Content is protected !!