August 16, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Chadema wavurugwa Dodoma

Spread the love

KUZUIWA kufanya mikutano ya kisiasa mkoani Dodoma, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeahaki, anaandika Dany Tibason.

Kutokana na hatua hiyo, Chadema kimepanga kuwafikisha mahakamani Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Mkuu wa Mkoa wa Dodoma (RC) pamoja na Mkuu wa Polisi Wilaya ya Dodoma Mjini (OCD).

Chama hicho kimetoa tamko hilo leo mkoani humo kutokana na kupigwa marufuku kuendesha mikutano ya hadhara wakati wa vikao vya Bunge.

Kauli hiyo imetolewa leo na Jella Mambo,  Mwenyekiti wa Chadema, Mkoa wa Dodoma alipozungumza na waandishi wa habari kutokana na madai ya kuchoshwa na unyanyasaji unaofanywa na viongozi wa mkoa kuzuia mikitano yao ya siasa ya wapinzani.

Mambo amesema kuwa, chama hicho kimepigwa marufuku na uongozi wa Mkoa wa Dodoma kufanya mikutano ya hadhara wakati wa vikao vya bunge.

Amesema, uongozi wa Chadema mkoa unakusudia kuwapeleka watu hao mahakamani ili mahakama iweze kutafusiri sheria na kasha kubaini kama kuna sheria yoyote ya masuala ya siasa kuzuia mikutano ya kisiasa wakati wa vikao vya bunge.

Mbali na hilo amesema, wanataka kujua kama kuna haki ya kuzuia mikutano ya kisiasa wakati wa vikao vya Bunge na iweze kufafanua kama sheria inahusu Mkoa wa Dodoma tu au na mikoa mingine.

“Utamaduni wa kuzuia mikutano ya kisiasa wakati wa vikao vya Bunge ulianzishwa na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk. Rehema Nchimbi jambo ambalo alilenga kufifisha upinzani Dodoma baada ya kuona kasi ya upinzani inapamba moto,” amesema Mambo.

Wakati wa Dk. Nchimbi, aliiandikia barua Chadema iliyokataza kuendesha mikutano ya hadhara katika kipindi cha Bunge na kwamba, inapingana na sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 1992.

“Lengo hapa ni kukandamiza upinzani ambao unaonekana kupanda chati kila siku, hivyo wanatunyima kufanya mikutano yetu kwa visingizio vya Bunge.

“Lakini ukiangalia sheria ya vyama vya siasa inasema kuwa moja ya majukumu ya vyama vya siasa ni kufanya mikutano na mambo mengine kama hayo bila kujali kuna bunge au hakuna,” amesema Mambo.

Amesema kuwa, lengo la kwenda mahakani ni kutaka kupatiwa tafsili ya sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 1992 ambayo itawasaidia kuondokana na kero hiyo ambayo imekuwa ikiletwa na watawala wa mkoa wa Dodoma ambao ni wateule wa chama cha mapinduzi.

“Huku ni kutaka kuipunguza nguvu chadema pamoja na upinzani kwa ujumla kwani wamekuwa wakitusumbua sana.

“Wengine tunapigwa na polisi lakini pia tunafunguliwa kesi zaidi ya tatu na tunashinda sasa hatutakiwi kuendelea na hali hii ndiyo maana tunataka kwenda mahakani ili kuweza kupatiwa tafsiri ya sheria hii,”amesema Mambo.

Amesema kuwa, kitendo cha Joshua Nasari Mbunge wa Arumeru mashariki kutolewa bungeni kwa kuvutwa kama mwizi alipotoa hoja ya msingi ya kutaka kujadiwa kuondolewa kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) ni unyanyasaji wa kijinsia na kumkosea adabu mtu ambaye ni mwakilishi wa wananchi.

error: Content is protected !!