Saturday , 25 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Chadema wataka  wahanga tukio la moto Kariakoo walipwe fidia
Habari za Siasa

Chadema wataka  wahanga tukio la moto Kariakoo walipwe fidia

Muonekano wa soko la Kariakoo baada ya kuungua moto
Spread the love

 

SERIKALI imeombwa iwalipe fidia wafanyabiashara waliopoteza mali zao katika tukio la moto uliounguza sehemu ya Soko Kuu la Kariakoo, jijini Dar es Salaam. Anariopti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Wito huo umetolewa leo Jumanne, tarehe 13 Julai 2021 na Kaimu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),  Kanda ya Pwani, Baraka Mwago, akizungumza na wanahabari mkoani Dar es Salaam.

Tukio hilo lilitokea usiku wa Jumamosi, tarehe 10 Julai mwaka huu na kusababisha  wafanyabishara zaidi ya 200, kupoteza mali zao kufuatia tukio hilo.

Mwago amesema kuwa, asilimia kubwa ya wafanyabiashara hawatakuwa na fedha za mtaji, hivyo inatakiwa wapatiwe msaada wa kifedha kwa ajili ya kuendelea na biashara zao.

“Wale wenye mikopo tujiulize itachukua muda gani kurudisha mkopo? Wengi tulioongea nao wanasema hawana fedha mali zao zote zimepotea. Hawana fedha taslimu, fedha yao yote walizungushia kuweka kwenye mali iliyopotea,”

https://youtu.be/P0i73cKNS-w

“Serikali inabidi ichukue hatua kupitia kadhia hii, tunawaomba  waone namna ya kuwalipa fidia wafanyabaishara wote waliopata majanga ya moto. Kwa jana tulivyoongea nao, soko lina wafanyabiashara wanaojuana wote, hivyo  wanajulikana Serikali iwalipe fidia,” amesema Mwago.

Baada ya tukio hilo kutokea, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, aliunda tume ya uchunguzi ili kubaini chanzo chake na athari za moto huo.

Tume hiyo inatarajia kumaliza kazi ya  uchunguzi Jumapili, tarehe 18 Julai mwaka huu.

Pia, Waziri Majaliwa aliziomba taasisi za kifedha ziwape muda wa ziada, wafanyabiashara wanaodaiwa, kulipa mikopo yao.

Akizungumzia hatua hiyo, Mwago amesema imeleta faraja kidogo kwa wafanyabiashara hao. “Waziri miuu alitoa neno la faraja aliposema benki zitoe muda ili waliokopa warejesha mikopo yao.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia aagiza iundwe kamati ya pamoja ya Mawaziri mradi wa BBT

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amewaagiza mawaziri kuunda kamati...

Habari za Siasa

Rais Samia apangua makatibu tawala mikoa, ateua Kamishna DCEA

Spread the loveALIYEKUWA Kamishna wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya, Gerald...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

M/kiti bodi ya wadhamini Chadema afariki dunia

Spread the loveMWENYEKITI wa Bodi ya Wadhamini ya Chama cha Demokrasia na...

Habari za Siasa

Zitto: Nikifa Ado atavaa viatu vyangu

Spread the love  KIONGOZI Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe...

error: Content is protected !!