Wednesday , 29 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Chadema, Wasira wapingana kuhusu serikali za majimbo
Habari za Siasa

Chadema, Wasira wapingana kuhusu serikali za majimbo

Freeman Mbowe, Mwenyekiti Chadema Taifa
Spread the love

 

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kupingana na mwanasiasa mkongwe nchini, Stephen Wassira, kuhusu Serikali za Majimbo, baada ya chama hicho kumueleza kwamba hajafanya utafiti kubaini faida zake licha ya kuendeshwa kwa gharama kubwa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Iringa … (endelea).

Jana tarehe 28 Februari 2023, akizungumza katika mkutano wa hadhara mkoani Iringa, Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe, alimueleza mwanasiasa huyo kwamba, Serikali za Majimbo ni muhimu kwa kuwa zinashusha madaraka kwa wananchi.

Mbowe alitoa kauli hiyo baada ya Wassira kupitia ukurasa wake wa Twitter, kupinga msimamo wa Chadema kutaka Tanzania kuanzisha Serikali za Majimbo, akisema zina gharama kubwa lakini pia zinahamasisha ukabila.

“Jana kaibuka Mzee wetu Wassira, anasema nimemsikia Mbowe anasema mambo ya Serikali ya majimbo zina gharama, sasa gharama na umaskini kipi kina afadhali? Anasema ni gharama lakini hawajafanya utafiti, hawa wanajua serikali za majimbo zinapeleka ulaji kwa Watanzania,” alisema Mbowe.

Mwenyekiti huyo wa Chadema alitetea hoja ya chama hicho dhidi ya Serikali za Majimbo akisema “tuna waziri mmoja wa elimu, nchi hii kubwa namna hii akikosea nchi nzima wanafeli. Tunaweka mayai yote kwenye kapu linaloitwa Serikali Kuu, Serikali za majiji zote ni omba omba kwa serikali sababu kodi zote zinazokusanywa kila mahali zinapelekwa kapu kuu la hazina wale wanagawa.”

“Chadema tunasema lazima tubadilishe mfumo huo tuanzishe Serikali za Majimbo kwani zinashusha madaraka ya maamuzi ya rasilimali za nchi kwenye madaraka ya jimbo,” alisema Mbowe.

Steven Wasira

Kufuatia majibu hayo ya Chadema kupitia kwa Mbowe, MwanaHALISI Online, leo tarehe 1 Machi 2023, imemtafuta Mzee Wasira kwa simu kwa ajili ya kupata maoni yake zaidi, ambaye amesema Tanzania haihitaji Serikali za Majimbo kwa kuwa ina Serikali za Mitaa ambazo zinatakiwa kuimarishwa zaidi kwa kuwa ziko karibu na wananchi kuliko mfumo wanaoupendekeza chama hicho.

Mzee Wassira amesema, nchi zinazotumia mfumo huo zinakabiliwa na mzigo mkubwa wa kuhudumia Serikali za Majimbo “ukitaka kuanzisha majimbo huwezi anzisha kama style, lazima uwe na sababu zinazoeleweka, sababu rasilimali zinapatikana katika mambo ya kitaifa ambayo tunatoza kodi.”

“Tuna bandari tatu, kodi zinazotokana na bandari hizo zinagawawiwa kwenda sawa nchi nzima. Tuna Serikali za Mitaa huko wilayani ambazo ziko karibu zaidi na wananchi kuliko serikali za majimbo ambazo ukiziunda zinakuwa mbali na wananchi,” amesema Mzee Wassira.

Mwanasiasa huyo mkongwe nchini amesema kuwa, baadhi ya mataifa yaliyoanzisha serikali za majimbo, walikuwa na sababu zilizotokana na historia yao, akitolea mfano Marekani iliyoanzisha Serikali za Majimbo kutokana na kuwa na muunganiko wa nchi 13.

1 Comment

 • A. UTANGULIZI
  1. Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja kwamba, Bunge lako Tukufu sasa lipokee na kujadili Taarifa ya Utekelezaji ya Mwaka 2022/23 na kupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Madini kwa Mwaka 2023/24.
  2. Mheshimiwa Spika, nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema kwa kuniwezesha kuwasilisha Hotuba hii muhimu mbele ya Bunge lako Tukufu. Aidha, kwa namna ya kipekee kabisa namshukuru Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuniamini kuendelea kusimamia Sekta ya Madini ili kufikia matarajio ya Watanzania katika Sekta ya Madini ya kuongeza mchango wake kwenye Pato la Taifa.
  3. Mheshimiwa Spika, vilevile kwa dhati nampongeza Mhe. Rais kwa namna anavyoiongoza Serikali ya Awamu ya Sita inayosimamia utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2020-2025, ambapo mafanikio mengi yamepatikana katika sekta mbalimbali ikiwemo Sekta ya Madini. Mafanikio hayo yameendelea kuitangaza nchi yetu siyo tu katika Bara la Afrika bali Duniani kote.
  4. Mheshimiwa Spika, ninaomba nitoe Rai kwa wananchi na Waheshimiwa Wabunge wote bila kujali itikadi za aina yoyote, tuendelee kuyaenzi mafanikio haya makubwa na kuendelea kushirikiana kwa pamoja katika kuchangia maendeleo ya kiuchumi na kijamii nchini.
  5. Mheshimiwa Spika, vilevile, nitumie fursa hii kuwapongeza na kuwashukuru Viongozi Wakuu wa Kitaifa, ambao ni Makamu wa Rais, Dr. Philip Isdor Mpango pamoja na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dr Hussein Ali Mwinyi kwa hekima kubwa katika kumsaidia Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuongoza nchi yetu.
  6. Mheshimiwa Spika, pia, nimshukuru na kumpongeza Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.) kwani amekuwa mstari wa mbele katika kusimamia na kufuatilia utekelezaji wa Ilani ya CCM na maelekezo mbalimbali ya Mhe. Rais pamoja na kusimamia vema shughuli za Sekta ya Madini ndani na nje ya Bunge.
  7. Mheshimiwa Spika, ninakushukuru wewe binafsi, Naibu Spika, Wenyeviti wa Bunge, Wenyeviti wa Kamati za Kudumu za Bunge, akiwemo Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Mhe. Dunstan L. Kitandula (Mb.) na Wajumbe wa Kamati hiyo. Kamati hii imefanya kazi nzuri na kutoa ushauri wa kuboresha mambo mbalimbali ikiwemo kupitia na kuchambua Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Madini na Taasisi zake kwa mwaka 2022/23.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

TEMESA iliyokarabati Kivuko kwa Bil 7.5 yapata hati chafu

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

ACT-Wazalendo yakusanya Mil 8.5/- kodi ya zuio na kutokomea nazo

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

DC Kasilda Mgeni ahamasisha chakula shuleni

Spread the love  MKUU wa Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, Kasilda Mgeni...

Habari za Siasa

Bilioni 223.9 zapelekwa Tunduru ndani ya miaka 2 ya SSH

Spread the love  ZAIDI ya Sh. bilioni 223.9 zimepelekwa Wilaya ya Tunduru...

error: Content is protected !!