August 13, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Chadema wapokwa kata Kibamba

Spread the love

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imemvua udiwani Ephraim Kinyafu, aliyekuwa Diwani wa Kata ya Saranga (Chadema) kwa madai uchaguzi uligibikwa na unakasoro, anaandika Faki Sosi.

Akitoa hukumu leo Warialandwe Lema, Hakimu Mkazi katika Mahakama ya Kisutu amesema kuwa, mlalamikaji Yusuph Mdoe (CCM),   aliyekuwa mpinzania wa Kinyafu alifungua kesi ya kutaka kubatilisha ushindi wa Kinyafu kutokana na kituo kimoja kukosewa kwa utatibu wa kuhesabu kura. Uchaguzi huo ulifanyika tarehe 25 Oktoba mwaka jana.

Katika matokeo ya uchaguzi huo, Kinyafu amemzidi Mdoe zaidi ya kura 500 ambapo kwenye kituo kinacholalamikiwa, wapiga kura hawakufika 70.

Kwa mujibu wa Fredick Kiwelu, Mwanasheria wa Chadema amesema kuwa, wataka rufaa katika kesi hiyo kutokana na hukumu iliyoamuriwa kurudiwa kwa uchaguzi kata zote wakati ni kata moja tu iliyo na kasoro, haipo sahihi.

Kiwelu amesema kuwa, katika shitaka hilo aliyepaswa kushurutishwa ni msimamizi wa kituo hicho cha kuhesabu kura.

 

error: Content is protected !!