Tuesday , 27 February 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Chadema waomba uhakiki wa daftari, Tume Huru
Habari za Siasa

Chadema waomba uhakiki wa daftari, Tume Huru

Mwenyekiti wa Kanda ya Pwani wa Chadema, Frederick Sumaye
Spread the love

CHAMA cha Chadema Kanda ya Pwani kimeikumbusha serikali kufanya uhakiki wa daftari la kupiga kura kwa muda muafaka ili kila mpiga kura apate haki ya kuandikishwa. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Hayo amesema Mwenyekiti wa Kanda hiyo, Frederick Sumaye akitoa maazimio ya Baraza Kuu la Chadema Kanda ya Pwani leo tarehe 24 desemba  2018 jijini Dar es Salaam.

“Tangu uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kuna mabadiliko yametokea kati ya idadi wapiga kura, hadi sasa kuna watu wamefikia umri wa kupiga kura lakini hawajaandikishwa, zoezi la kuandikisha wapiga kura linatakiwa lifanyiwe kwa muda muafaka.

“Tunasema hivyo kwa sababu mwaka kesho ni mwaka wa uchaguzi mdogo, zoezi hilo litakalofika baraza linakumbusha kila mtu apate kadi ya kupigia kura kwa wale ambao watakuwa na haki ya kupiga kura,” amesema Sumaye.

Vile vile, Sumaye amesema kuelekea mwaka wa uchaguzi wa 2020, baraza hilo linaitaka serikali kuunda tume huru ya uchaguzi haraka kabla uchaguzi huo haujafika

“Azimio lingine, kwa ajili ya mapungufu yaliyopo katika muundo mzima wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) tume huru ya uchaguzi ambayo haitapewa maelekezo ya utawala na kuwa na watumishi wake pasipo kutegemea watumishi wa serikali iundwe haraka kabla ya uchaguzi ujao,” amesema Sumaye.

Katika hatua nyingine, Sumaye amewataka wananchi hasa wapenda mabadiliko kutokata tamaa ya kupiga kura pindi kipindi cha uchaguzi kitakapofika, bali wajitokeze kwa wingi ili kura zao zibadilishe mfumo uliopo.

“Wapo wapenda mabadiliko ambao inaonekana wamekata tamaa  kuwa hakuna haja ya kupiga kura sababu matokeo yanajulikana kabla ya kupigwa kura kwa sababu ya matumizi ya nguvu za dola na maelekezo ya tume ya uchaguzi kutoka serikali ya CCM. Kupambana na hilo ni kujitokeza kwa wingi kupiga kura na si vinginevyo,” amesema Sumaye.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Hamahama Ngorongoro kutikisa maandamano ya Chadema Arusha

Spread the loveMAELFU ya wanachama na wafuasi wa Chama cha Demokrasia na...

Habari za SiasaTangulizi

Waliofariki ajalini Arusha kuagwa siku ya maandamano Chadema

Spread the loveMIILI ya watu 25 waliofariki dunia katika ajali iliyohusisha lori...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali kuiburuzwa mahakamani ajali iliyoua 25 Arusha

Spread the loveMTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), imeitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Samia atoa pole ajali iliyoua 25, kujeruhi 21 Arusha

Spread the loveRais Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za rambirambi kwa Mkuu...

error: Content is protected !!