Saturday , 15 June 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Chadema wamweka kwenye kona IGP Sirro
Habari za Siasa

Chadema wamweka kwenye kona IGP Sirro

Spread the love

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimempa mtihani mzito Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Kimemtaka aache kulalama badala yake afumue mfumo wa jeshi hilo, ili kuondoa upungufu uliopo.

Wito huo wa Chadema umetolewa leo tarehe 25 Septemba 2019, kupitia Tumaini Makene, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa chama hicho.

Ni siku moja baada ya IGP Sirro kueleza kwamba, anatamani akimaliza muda wake, aliache Jeshi la Polisi likiwa na heshimika.

Taarifa ya Chadema imeeleza kuwa, ili IGP Sirro atimize ndoto yake hiyo, anatakiwa kufanya mabadiliko makubwa ya kimfumo katika jeshi hilo, kuanzia kwenye mitaala ya mafunzo, sheria na utendaji kwa ajili ya kuwa chombo kinachotoa huduma babala ya kuwa chombo cha mabavu.

“Chadema kinatoa wito kwa IGP Sirro kufanya mabadiliko ya kimfumo, kwa ajili ya kulifanya kuwa chombo kinachotoa huduma badala ya chombo cha mabavu kama ilivyo sasa.

“..Ili kudhihirisha nia yake ya kutamani kuliacha jeshi hilo likiwa na heshima,” inaeleza taarifa ya Chadema.

Aidha, Chadema imemuomba IGP Sirro alielekeze Jeshi la Polisi nchini kutimiza wajibu wake kwa mujibu wa sheria, kwa kushughulikia matukio mbalimbali yakiwemo ya watu kupotea, kushambuliwa, kutekwa, kuteswa na wengine kuokotwa wakiwa wamekufa.

“IGP Sirro alielekeze Jeshi la Polisi kushughulikia matukio mbalimbali kwa kufanya uchunguzi, kuwabaini watuhumiwa na kuwafikisha mbele ya sheria.

“Kwa kuanzia ili kuondoa picha mbaya waliyonayo wananchi dhidi ya chombo hicho, wafanyie kazi tukio la kushambuliwa Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu,” inaeleza taarifa ya Chadema na kuongeza;

“Tukio la kupotea mwanahabari Azory Gwanda, kutowekwa kwa Msaidizi wa Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Bernard Saanane na kuanzisha uchunguzi wa tukio la kuuawa kwa kupigwa risasi aliyekuwa mwanafunzi wa Chuo cha Usafirishaji cha Taifa (NIT), Akwilina Akwiline.”

Chama hicho kimeshauri kuwa, ni vyema IGP Sirro ajielekeze kuhakikisha Jeshi la Polisi linajikita kwenye mabadiliko kwa vitendo vinavyoonekana, ambavyo vitadhihirisha nia na uthabiti wa matamanio yake ya kuliacha jeshi hilo likiwa na heshima.

“Msimamo wa kisera wa Chadema ni kuona Jeshi la Polisi linafanyiwa mabadiliko ya kimfumo, kulipatia taswira chanya ili kuwa kimbilio la ulinzi na usalama wa raia na mali zao.

” Si kuwa chombo cha kutia hofu jamii kwa ajili ya kulinda chama kilichoko madarakani kwa sasa,” kimeeleza Chadema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Tanesco yawasha mtambo namba 8 Bwawa Julius Nyerere

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Samia: Wakuu wa mikoa, wilaya wanaendeleza ubabe

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amesema bado wakuu wa wilaya na...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Ramaphosa achaguliwa tena kuwa rais Afrika Kusini

Spread the loveRais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa amechaguliwa na wabunge wa...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

DA, ANC waridhia kuunda serikali ya mseto Afrika Kusini

Spread the loveChama tawala nchini Afrika Kusini cha African National Congress, ANC,...

error: Content is protected !!