Sunday , 5 February 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Chadema wamvaa Nape, “asiturudishe zama za giza”
Habari za SiasaTangulizi

Chadema wamvaa Nape, “asiturudishe zama za giza”

Nape Nnauye, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Tekinolojia
Spread the love

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimemtaka Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia na Habari, Nape Nnauye aviache vyombo vya habari vitimize wajibu wake kuhusu suala la mikutano ya hadhara ambayo tarehe 21 na 22 Januari mwaka huu chama hicho kitaizindua rasmi katika mikoa ya Mwanza na Mara.

Pia kimemtaka aheshimu kauli ya Rais Samia Suluhu Hassan kwamba wanaCCM wanatakiwa kujibu hoja zinazoibuliwa kwenye mikutano hiyo ya hadhara kwa hoja. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Hayo yamejiri baada ya wiki iliyopita Nape kuviasa vyombo vya habari akiviasa vyombo vya habari kwamba vi-balance taarifa zinazoibuka kwenye mikutano ya hadhara kuhusu serikali.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo tarehe 15 Januari, 2023, Mkurugenzi wa Mambo ya Nje, Itikadi na Uenezi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mrema amesema kauli hiyo ya Nape imetoka wakati si sahihi.

“Nape anataka kuturudisha kwenye usiku wa giza ambapo tunapambana kutoka huko kwenda kwenye mwanga. Kauli hii ni malengo yake ni kuvitisha vyombo vya habari visirushe mikutano mubashara kwa sababu kama unarusha mubashara utapata wapi fursa wa kwenda kubalansi hiyo stori serikalini?

“Nape atuachie, rais samia ameshasema amewambia wanachama wa chama chake wakajibu hoja, nape aviache vyombo vya habari vifanye kazi yake kwa uhuru visirudi kule tulipotoka kwenye zama za giza,” amesema.

Aidha, ameviomba vyombo vya habari visiwe na hofu kwa sababu siku zote wao huzungumza kwa hoja.

“Mikutano yetu inaendeshwa kwa hoja na ajenda mahsusi, tunamtaka waziri wa habari aviache vyombo vya habari vitimize wajibu wake, vyama vya siasa vitimize wajibu wake, ili tuende sasa tukajenge Taifa kwa pamoja kwa mshikamano bila vitisho, bila kurudishana nyuma kwa sababu zama hizo za giza tunapambana kutoka huko kuingiza zama za mwanga,” amesema.

Aidha, amesema maandalizi ya kurejea kwa Makamu Mwenyekiti wa chama hicho bara, Tundu Lissu yanaendelea vizuri na vyombo vya habari vitapewa rasmi taratibu na njia atakayopita.

“Suala la mapokezi yatakuwaje, jukumu hilo litafanywa na uongozi wa kanda ya Pwani mapema iwezekanavyo. Ngazi ya taifa tunaenda Mwanza na Musoma tarehe 21 na 22 hatimaye tutarudisha Dar es Salaam kuja kushirikiana na viongozi wa kanda ya Pwani katika maandalizi na mapokezi ya kiongozi wa chama chetu,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo aungana na wananchi ujenzi maabara za sekondari

Spread the loveMBUNGE wa Musoma Vijijini, Profesa Sospeter Muhongo, kwa kushirikiana na...

Habari MchanganyikoTangulizi

Haya hapa majina 12 ya familia moja waliofariki kwenye ajali Tanga

Spread the love  MAJINA 12 kati ya 17 ya waliofariki dunia katika...

Habari za Siasa

CCM apiga marufuku wazazi kuwatumia watoto wa kike kwenye mambo ya kimila

Spread the loveKATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Daniel Chongolo...

Habari za Siasa

Ofisi za mabalozi wa mashina zitumike kuwale vijana kimaadili – Chongolo

Spread the loveKATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo ameagiza...

error: Content is protected !!