August 17, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Chadema wamkemea JPM

Rais John Magufuli

Spread the love

KAULI ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  John Magufuli kuwa wakati wa utawala wake hakuna wanafunzi wataopata ujauzito wataruhusiwa kurejea masomoni baada ya kujifungua imeelezwa kuwa ni chuki ya wazi kwa wanawake na watoto, anaandika Victoria Chance.

Rais Magufuli alitoa kauli hiyo tarehe 22 Juni, mwaka huu akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Pwani, huku kauli yake ikiungwa mkono na Ummy Mwalimu, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto pamoja na Mwigulu Nchemba, Waziri wa Mambo ya ndani.

Akizungumza kwa niaba ya Baraza la Wanawake wa Chadema, Halima Mdee ambaye ni mwenyekiti wa baraza hilo amesema “Mawaziri walionekana kama waliunga mkono tamko la Rais  ni kwasababu ya hofu ya kumuogopa mwenyekiti wao wa chama ambaye pia ni Rais.

“Mjadala huu unaohusu watoto wa kike kutokurudi shule hautofungwa kwasababu Rais  amesema au waziri amesema. Kwasababu neno la Rais sio sheria.”

Mdee amedai kwamba Rais asirudishe  nchi miaka ya arobaini na nane (1948), kipindi ambacho hakukuwa na mikataba wala nyaraka yoyote kuhusiana na watoto.

“Rais anatakiwa kufunga ‘breki’ kutokana na kwamba nchi hii inaendeshwa kwa Katiba na mikataba mbalimbali ya kimataifa,” amesema.

Mbunge huyo ambaye kitaaluma ni mwanasheria na wakili wa Mahakama Kuu amesema sera ya elimu ya Tanzania ipo wazi kuhusu fursa ya wanafunzi kurudi shule baada ya kupata ujauzito na kujifungua kabla ya kuhitimu masomo.

“Rais anachotaka kufanya ni kuvunja mikataba mbalimbali  ya kimataifa inayohusu watoto. Tuna mkakati wa kufungua mashtaka kuhusiana na jambo hilo kwani ni kinyume cha sheria na pia ni uvunjifu wa haki  za binadamu,” amesema Mdee.

error: Content is protected !!