January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Chadema wamavaa Magufuli uchaguzi wa meya

Spread the love

CHAMA Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimemtaka Rais John Magufuli kutumbua majipu yaliyopo ofisini kwake kutokana na watumishi wa serikali kutumika kuvuruga chaguzi za mameya kwenye miji mbalimbali nchini. Anaandika Faki Sosi … (endelea).

Hayo yameelezwa leo Jijini Dar es Salaam na Ofisa Habari wa chama hicho, Tumaini Makene alipozungumza na waandishi wa habari na kwamba, katika maeneo mengi ya chaguzi ambayo vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kuwa na nafasi ya kutwaa umeya wa Halmashauri au Jiji, CCM hufanya vurugu.

Amesema kuwa, ofisi ya rais yenye sifa ya ‘kutumbua majipu’, inapaswa kutumbua majipu yanayohitajika kutumbuliwa licha ya kuwa yeye mwenyewe anaweza kuhusika kwenye zoezi hilo.

“Vurugu hizo zinaratibiwa kwenye ofisi ya rais kama sio rais mwenyewe kuhusika. Cha kushangaza halichukulii hatua suala hilo ambapo tunapata mashaka ya kuhusika kwake kwenye vurugu hizo kutokana na kuwa mambo hayo yanaendelea kwenye ofisi yake,” amesema Makene.

Amesema kuwa, Jiji la Tanga tangu jana limekuwa likizuungukwa na polisi wa doria wenye risasi na mabomu hali ambayo inawatia hofu wakazi wa jiji hilo.

Amesema kuwa, Jeshi la Polisi limekuwa na tabia ya kukilinda Chama cha Mapinduzi (CCM) ambao wamejijengea tabia ya kutumia jeshi hilo kulinda maslahi yao binafsi.

Wakati huo huo Makene amesema kuwa, Chadema inalaani uvunjwaji wa matawi ya chama chao na ushushwaji wa bendera unaoendele kwenye Jimbo la Ruangwa kwa kile kinachodaiwa kuwa ni amri ya Waziri Mkuu, Majaliwa Kassimu ambaye ni mbunge wa jimbo hilo.

Majaliwa amewekwa jimboni mwake katika kile kilichoelezwa kuwa yupo kwenye mapunziko ya siku 10 jimboni humo.

Makene amesema kuwa, vitendo hivyo ni viashiria vya ukandamizaji wa demokrasia na haki za wananchi ambapo waziri mkuu ameamuru watu kuchochea fujo kwa kuwataka wasiwe wafuasi wa chama kingene cha siasa ambapo ni kinyume na cha haki.

error: Content is protected !!