Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Chadema walia na wazee
Habari za Siasa

Chadema walia na wazee

Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Chadema, Rodrick Lutembeka
Spread the love

 

BARAZA la Wazee la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), limeiomba Serikali kuimarisha utolewaji wa huduma za afya kwa wazee, kwa kuwa kundi hilo linakabiliwa na matatizo ya kiafya. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Wito huo umetolewa leo Jumamosi, tarehe 18 Desemba 2021 na Katibu Mkuu wa baraza hilo, Roderick Lutembeka, katika uzinduzi wa rasimu ya sera ya wazee ya Chadema, jijini Dar es Salaam.

Lutembeka amesema, uchambuzi wa Sera ya Wazee ya Taifa ya 2003, unaeleza kwamba, wazee wengi huwa na afya dhaifu kwa sababu ya kupata magonjwa nyemelezi kutokana na matunzo duni wakati wa ujana wao.

“Kwa wazee walio wengi pamoja na ukweli huo, huduma za afya hazipatikani kwa urahisi kwa wazee walio wengi na mara nyingi huduma hizo ni ghali, watumishi wa afya wanaohudumia wazee hawaonyeshi muamko na hawana mafunzo ya kutosha katika eneo hili la kuwahudumia wazee,” amesema Lutembeka.

Wakati huo huo, Lutembeka ameshauri wazee wawe na watumishi wa kuwatunza ili kuwaepusha na ajali zinazoweza kuwapata kutokana na matatizo yao, kama uoni hafifu, kushindwa kupata hisia na kusikia.

“Yote haya ni sababu kubwa ya kuwepo matarajio ya kuwekeza katika wazee kuwa na watu wa kuwatunza nyumbani au kuwa na vituo maalum vya matunzo kwa wazee pale wanapofikia mahali wanahitaji kusaidiwa kutoka kitandani au nje ya nyumba wanazokaa,” amesema Lutembeka.

Katibu Mkuu huyo wa Wazee wa Chadema, amesema kundi hilo liko hatarini kupata ulemavu kutokana na umri wao.

“Utafiti uliochapishwa katika majarida ya kitaaluma na yanayokuliwa na Shirika la Afya Duniani (WHO), yanathibitisha kuwa, viwango vya kuishi na ulemavu huongezeka kadri umri unavyoongezeka kuanzia umri wa miaka 60 na kuendelea ,”

“Kutokana na sababu za kibaiolojia utendaji kazi wa viungo vya binadamu kama macho, pua, viganja na vidole na kuhusiana na uwezo na ubora kuhusiana na uwezo wa kuona, kupata hisia na vionjo hupungua. Mapungufu haya huchangia mazingira ya kuongezeka kwa ajali hivyo kujiweka wazi kwa ajali za moto na kuchomwa kwa vitu vyenye ncha kali.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Chadema yamtaka Rais Samia aunde tume kuchunguza mauaji mgodi wa Barick

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, ameombwa aunde tume huru kwa...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

error: Content is protected !!