Sunday , 2 April 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Chadema wakabiliana na Polisi Kinondoni
Habari za SiasaTangulizi

Chadema wakabiliana na Polisi Kinondoni

Wanachama wa Chadema wakiwa katika maandamano huku Polisi wakiwa tayari kuwakabili
Spread the love

VURUMAI kubwa imeibuka jijini Dar es Salaam, jioni hii, kufuatia jeshi la polisi kutumia mabomu ya machozi, risasi za moto na maji ya kuwasha kukabiliana na wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Anaripoti Faki Sosi… (endelea).

Vurugu hizo zilitokana na hatua ya wafuafi wa chama hicho, kuamua kutembea kwa miguu, kutoka Mwananyamala, kuelekea kwenye ofisi ya msimamizi wa uchaguzi jimbo la Kinondoni, kudai fomu za viapo kwa mawakala wake.

Taarifa kutoka kwa mashuhuda wa tukio hilo na ambazo hazikuweza kuthibitishwa mara moja zinasema, katika vurumai hiyo, watu wawili wanaweza kuwa wamefariki dunia na wengine kadhaa kujeruhiwa.

Wafuasi wa Chadema walianza kutembea kutoka uwanja wa Buibui, Kinondoni, muda mfupi baada ya mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, kumaliza kuhutubia mkutano wa hadhara na kuwataka kufanya hivyo.

Akizungumza kwenye mkutano huo, Mbowe aliwataka wananchi waliohudhuria mkutano huo kuwa msimamizi wa uchaguzi wa jimbo la Kinondoni amegoma kutoa fomu za viapo vya mawakala wa chama hicho kwa ajili ya uchaguzi wa kesho.

Viongozi wa juu wa Chadema akiwemo Mbowe, Vincent Mahinji (katibu mkuu); waziri mkuu mstaafu, Fredrick Sumaye; mbunge wa Kawe, Halima Mdee, John Mnyika (Naibu Katibu Mkuu-Bara) na mbunge wa Tarime Mjini, John Heche, ni miongoni mwa waliokuwa wakitembea kwenda kwenye ofisi hizo.

Wengine waliokuwa wakitembea kwa miguu, ni mgombea ubunge wa jimbo hilo, Salum Mwalim, viongozi wa ngazi mbalimbali kutoka kwenye wilaya na mikoa, walitembea kuelekea Magomeni, zilizopo ofisi za msimamizi huyo wa uchaguzi.

Mara baada ya wananchi na viongozi wa Chadema kutembea kwa miguu kutoka uwanja wa Buibui, mpaka Mkwajuni, askari polisi wakiwa katika magari zaidi ya matano waliweka kizuizi na kuanza kupiga mabomu kuwatawanya wananchi hao.

Katika hekaheka hizo, mwandishi alishuhudia wananchi zaidi ya 30 wakitiwa nguvuni huku baadhi yao wakijeruhiwa vibaya kwa vipigo kutoka kwa askari waliojihami kwa silaha za moto.

Kufuatia vipigo vizito vilivyoelekewa kwa baadhi ya wananchi, askari hao waliita gari ya kubebea wagonjwa (ambulance), ambayo ilibeba baadhi ya watu na kuondoka nao kuelekea eneo ambalo halikufahamika mara moja na mwandishi.

Kumekuwa na mvutano mkubwa kati ya msimamizi wa uchaguzi wa jimbo la Kinondoni, Aron Kagurumjuli na chama hicho, juu ya fomu za mawakala.

Kampeni za uchaguzi wa mbunge wa jimbo la Kinondoni zimehitimishwa leo, huku uchaguzi ukitarajiwa kufanyika kesho, Jumamosi ya tarehe 16 Februari 2018.

Uchaguzi huu, unafanyika ili kuziba nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Maulid Mtulia (CUF).

Mtulia aliamua kujiuzulu nafasi hiyo, mwishoni mwa mwaka jana kwa kile alichoita, “kumpenda sana Rais John Pombe Magufuli.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia apangua mawaziri

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan, amefanya mabadiliko madogo ya Baraza la...

Habari za Siasa

RC mstaafu afariki dunia, CCM yamlilia

Spread the loveALIYEWAHI kuwa mkuu wa mikoa ya Dodoma, Mara, Mtwara na...

Habari za Siasa

Marekani kuwekeza Dola 500 Mil kupeleka bidhaa na huduma Tanzania

Spread the loveMAKAMU wa Rais wa Marekani, Kamala Harris amesema miongoni mwa...

Habari za Siasa

Kamala ataja hatua mpya kuimarisha uhusiano wa kibiashara Tanzania, Marekani

Spread the loveKATIKA kuimaridha uhusiano wa kibiashara na kiuchumi baina ya Tanzania...

error: Content is protected !!