September 29, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Chadema: UVCCM mbumbumbu

Spread the love

UDHAIFU katika kutambua masuala ya kiuongozi kunaufanya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) kwenda hovyo, anaandika Dany Tibason.

Kauli hiyo imetolewa jana na Patrobas Katambi, Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa Chadema (BAVICHA) ambapo amewataka UVCCM kurudi darasani ili kujifunza masuala uongozi.

Amesema, vijana hao wanafanya siasa za kitoto kutokana na kukosa misingi ama hekima za kiuongozi.

Katambi ametoa kauli hiyo kutokakana na tamko la UVCCM la ‘kuwatusi’ viongozi wa dini pamoja na asasi nyingine kwa kuwataka kutojihusisha katika mazungumzo ya kumshauri rais juu ya mwenendo wa kisiasa nchini.

Katambi amesema, UVCCM ni watoto kwa kuwa, wanaropoka maneno ambayo hawayajui hasa pale wanapowabeza viongozi wa dini pamoja na taasisi mbalimbali ambazo zinatafuta usuluhishi wa kisiasa nchini.

“Vijana wa UVCCM bado ni watoto wadogo lakini pia wanatakiwa kupelekwa shule wakasome kwanza ili waache kuropoka. Tamko lao la juzi lilikuwa na maneno mengi ambayo yanaonesha kuwa viongozi hao ni watoto.

“Mtu mwenye akili hawezi kuhoji na kujenga mashaka heti Chadema hawakuzungumza na viongozi wa dini na taasisi mbalimbali ili kusitisha maandamano ya Ukuta ili kuruhusu mazungumzo kati ya viongozi wa dini na taasisi kuzungumza na rais.

“Sasa wanataka viongozi wa dini watajwe ili iweje na wakiwajua hao viongozi wanataka kuwafanya nini, sisi tunachokiangalia siyo kumtaja mtu bali ni kuangalia amani inapatikana kwa njia gani,” amesema na kuongeza;

“Siasa siyo kuropoka na kupiga kelele, siasa ni kujenga hoja kwa mafanikio ya taifa kwa ujumla na sio ujinga kama unaofanywa na UVCCM.”

Hata hivyo, amesema kwa sasa Watanzania wanatambu na kujua nani kichaa, nani mkweli na ni nani ambaye anamkandamiza mwingine.

Kutokana na hali hiyo Katambi amesema, haoni sababu ya kuendelea kuwajibu UVCCM.

error: Content is protected !!