Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Chadema: Tumemshtukia JPM
Habari za Siasa

Chadema: Tumemshtukia JPM

Rais John Magufuli
Spread the love

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimedai kushtukia ujanga unaotaka kufanywa na Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuelekea Uchaguzi Mkuu ujao. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma…(endelea).

 Akizungmza na wandishi wa habari jijini Dodoma leo tarehe 6 Mei 2019, Suzan Kiwanga, Mbunge wa Jimbo la Mlimba ambeye pia ni Waziri Kivuli Wizara ya Maji amesema, wanafahamu mtego uliouwekwa na Rais wa Awamu ya Tano kwamba, ataongeza mshahara Mei 2020 ili kuwazubaisha wananchi kuelekea Uchaguzi Mkuu.

“Hii ni rushwa ya uchaguzi, hawezekani kipindi chote hichi asiongeze mshahara, aje kuhongeza mishoni kipindi tunaelekea kwenye uchaguzi. Hili hatutalifumbia macho,” Amesema Kiwanga. 

Akihutubia katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) jijini Mbeya tarehe 1 Mei 2019, Rais Magufuli alisema, serikali inakabiliwa na changamoto ya gharama za uendeshaji, mishahara ya watumishi, deni la taifa, ma kutekeleza miradi ya maendeleo huku akiahidi kuwaongezea mishahara watumishi kabla ya kundoka madarakani.

“Gharama za kuendesha serikali bado ni kubwa, tunatumia takribani Sh. 580 Bil, kulipa mishahara kila mwezi, kwa bahati nzuri siku hizi tunalipa tangu tarehe 19 suala ambalo lilikuwa halipo, najua hili tungelipa hata tarehe 2 msingeshangilia,” amesema Rais Magufuli na kuongeza;

“Lakini pamoja na kwamba tunalipa kila mwezi, bado hicho kiasi kilichobaki tunatakiwa kulipa madeni ya mkopo. Tunatakiwa pia tushughulikie miradi ya maendeleo hivyo mnaweza kuona wenyewe tunatumia kiasi gani, na kinachobaki tumekuwa tukijiuliza tukipeleke wapi.”

Kwenye mkutano na wanahabari Devotha Minja, Waziri Kivuli wa Habali, Utamaduni, Sanaa na Michezo ameeleza kushangazwa na kauli ya kutopandisha mishahara wafanyakazi huku takwimu za makusanyo ya kodi zikielezwa kupanda.

Hata hivyo amesema, takwimu zinanaonesa kuwa, Tanzania inazidi kushuka kati ya nchi ambazo wananchi wake wasio na furaha na kwamba, yapo mengi ya kujiuliza.

“Lipi la msingi? hili la kuingiza fedha kwenye miradi mikubwa na kuwaacha watumishi wakiwa na hali ngumu ya kimaisha?” Amehoji na kuongeza;

“Kama kwa mwezi tunaweza kukusanya Shilingi Trilioni 1.3, halafu uwapi motisha? Huku ni kuwanyong’onyeza watumishi wa umma na kuzorotesha utendaji kazi.”  

Ruth Mallel, Waziri Kivuli wa Utumishi na Utawala Bora amesema, hakuna serikali inayoweza kufikia uchumi wa kati ikiwa inazuia kupandisha mishahara ya watumishi wa umma.

Mollel ambaye ni Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Pwani kupitia Chadema amesema, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaamini kwamba, Serikali ya Awamu ya Tano haiwezi kufikia uchumi wa viwanda kama maslahi ya watumishi wa umma hayataboreshwa.

Amesema, inasikitisha kwamba, kinyume na matarajio ya watumishi wa umma nchini pamoja na uchumi kukua na makusanyo ya kila mwenzi kuongezeka, hadi kufikia Sh. 1.3 trilioni lakini hakuna nyongeza wala marekebisho ya mshahara amabayo ni haki ya watumishi wa umma kisheria.

“Nyongeza za mishahara ni stahili ya mtumishi ambaye anapata kwenye wigo wa mshahara na nyongeza, hiyo inafafanuliwa kwenye kanuni za utumishi wa umma (SOE8) ambayo kawaida ni kati ya shilingi 10,000 na 20,000 kutegemea  na ngazi ya mshahara wa afisa.

“Sisi Kambi Rasmi ya Upinzani tumekuwa tukiwasumbua mawaziri kuhusiana na jambo hili, na jibu tuliyokuwa tukiyapata ni kwamba mishahara haitopandishwa mpaka kukamilika kwa miradi mikubwa ambayo itachukuwa muda mrefu,” amesema Mollel.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

error: Content is protected !!