Tuesday , 18 June 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Chadema, serikali wavimbiana
Habari za Siasa

Chadema, serikali wavimbiana

Spread the love

SERIKALI mkoani Simiyu imepiga marufuku kufanyika Mkutano wa ndani wa Chama cha Demkrasia na Maendeleo (Chadema) kesho tarehe 21 Oktoba 2018, hata hivyo chama hicho kimesema kitafanya. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Mkutano wa ndani wa Chadema umeelezwa kujikita zaidi katika ujenzi wa chama baada ya kuamua kususia chaguzi zote zitazotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini (NEC).

Chadema ilipanga kufanya mkutano wa ndani wa kujenga chama wilayani Bariadi, Simiyu ambao utahudhuriwa na viongozi wa Kamati Kuu, viongozi wa kanda hiyo (Simiyu, Mara na Shinyanga) na wanachama.

Festo Kiswaga, Mkuu wa Wilaya ya Bariadi amezungumza na wanahabari na kueleza kuwa, Chadema haijatoa taarifa ya kufanyika mkutano huo kwa Jeshi la Polisi na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya kama taratibu zinavyoeleza.

Na kwamba, wajumbe kati ya 500 na 1000 wanatarajiwa kuhudhuria mkutano huo akiwemo Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye lakini taarifa ya kikao hicho na malengo yake haijatolewa.

“Sijaambiwa chochote hivyo natilia shaka kwanini wasitoe taarifa ili tutoe ulinzi,” amesema na kuongeza kuwa, ndani ya mkutano huo kuna agenda mbalimbali ambazo hazina masilahi na wananchi wa Bariadi na Simiyu.

Mkuu huyo ameeleza kuwa, siku hizo za kikao mkoani mkoani humo kutakuwa na maonesho ya Sido na kwamba, kwenye wilaya hiyo kwa sasa wanahitaji maendeleo.

Amesema, maonesho hayo yatahudhuriwa na viongozi wengi wa serikali akiwemo Kasim Majaliwa, Waziri Mkuu hivyo polisi hawawezi kujigawa katika ulinzi.

John Mrema, Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje Chadema amesema kuwa, kikao kitafanyika kama kawaida na kwamba, Mkuu wa Wilaya hana mamlaka ya kuzuia mkutano huo.

Akifafanua zaidi Mrema amesema, ajenda za kikao chao ni kujiandaa na chaguzi za ndani ya chama na kuwa, wajumbe wake hawatofika 500 kama ilivyoelezwa na Kiswaga.

“Mkuu wa Wilaya hana mamlaka ya kupiga marufuku mkutano wa ndani, mkutano huo ni haki yetu, hutuanzii Simiyu, tunafanya kanda zote, lengo ni kukipanga chama kuelekea uchaguzi wa ndani ya chama, huo ni mkutano halali,” amesema Mrema huku akimtuhumu Kiswaga kutojua sheria ya vyama vya saisa.

“Mkutano wa ndani hauombewi kibali, anatumia sheria gani? Akasome sheria ya vyama vya siasa, pia hakuna mahali sheria ya vyama vya siasa inapomtambua mkuu wa wilaya,” aamesema Mrema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Mazingira magumu ya JPM yamechangia ‘Comedy Journalism’

Spread the loveMwenyekiti wa Kamati ya kufuatilia hali ya uchumi wa vyombo...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

RC Chalamila: Nimeacha ubabe

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chamalila amemthibishia...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Rais Samia atoa ujumbe mzito Sikukuu Eid Al Adha

Spread the loveKATIKA kusherehekea Sikukuu ya Eid Al Adha, Rais wa Tanzania,...

BiasharaHabari za Siasa

Dk. Biteko aipongeza NMB kwa kuanzisha utoaji wa bima ya mifugo

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!