Saturday , 2 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Chadema Pwani: Ni zamu ya CCM kudondosha chozi
Habari za Siasa

Chadema Pwani: Ni zamu ya CCM kudondosha chozi

Spread the love

CHAMA cha Demokraia na Maendeleo (Chadema), Kanda ya Pwani kimesema, ni zamu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kudondosha chozi. Anaripoti Hamisi Mguta, Dar es Salaam…(endelea).

Hayo yamesemwa na kaimu mwenyekiti wa kanda hiyo, Baraka Mwango leo Jumatatu tarehe 13 Julai 2020 wakati akifungua mkutano mkuu wa Jimbo la Segerea wenye lengo la kupiga kura za maoni za ubunge.

Wanachama watano wamejitosa kuwania kupeperusha bendera za Chadema kwenye uchaguzi mkuu wa Oktoba 2020. Mbunge anayemaliza muda wake ni Bonnah Kamoli wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Waliojitosa kwenye mbio hizo ni Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema, Gango P. Kidela, Masato Wasira, Agnesta Lambert na  Andrew Kimbombo.

Mwango amesema, mmoja kati ya wanachama hao, anatarajiwa kupeperusha bendera ya chama hicho katika jimbo hilo huku akisisitiza, kilichookea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 na kusababisha wapinzani kupiga yoye, kitatokea kwa CCM.

“Hatujawahi kushinda uchaguzi kwa huruma ya CCM wala Tume Huru, hakuna uchaguzi huru Tanzania bali tuna Tume ya Uchaguzi, tunashinda kwasababu ya nguvu ya umma, safari hii hatutaweza kulalamika ila na wao ndio wakalalamika.”

“Tumemsikia Mzee Wasira (Steven Wassira aliyekuwa mgombea wa Bunda-Mjini) alisema uchaguzi wa mwaka 2015 Bunda haukuwa huru na haki, sasa tunataka hivyo vilio vililiwe nchi nzima, sio Bunda peke yake, safari hii CCM watalia maeneo yote,”amesema.

Akizungumzia kuhusu ushirikiano na vyama vingene, Mwago amesema, kila chama kiliundwa kwa lengo la kushika dola.

“Kila chama kina mikakati yake ya kujiandaa kushinda, kwa Chadema hakiishi kwa mikakati ya chama kingine,” amesema.

Chadema leo kinatarajia kumpata mgombea wake katika jimbo la Segerea ambapo wagombea wote watano wameshajinadi huku wajumbe wa mkutano huo, wakijiandaa kupiga kura.

Endelea kufuatilia MwanaHALISI Online na MwanaHALISI TV kujua kitakachiojili 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia kuzindua programu ya nishati safi ya kupikia kwa wanawake Afrika

Spread the loveRais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuzindua programu ya...

Habari za Siasa

AG aiagiza kamati ya maadili kuwashughulikia mawakili wanaokiuka maadili

Spread the loveMWANASHERIA Mkuu wa Serikali (AG), Dk. Eliezer Feleshi, ameagiza Kamati...

Habari za Siasa

Jaji avunja ukimya sakata la Mpoki kusimamishwa uwakili

Spread the loveJAJI Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Juma, amekitaka Chama cha...

Habari za Siasa

Sheikh Ponda ataka mwarobaini changamoto uchaguzi 2020

Spread the loveKATIBU Mkuu wa Shura ya Maimamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa...

error: Content is protected !!