January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Chadema: Miswada hii iondelewe bungeni

Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika

Spread the love

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimewataka wabunge wanaounda Umoja wa Kutetea Katiba ya Wananchi (UKAWA), kukwamisha miswada mine itakayowasilishwa bungeni katika mkutano wa 19 unaoendelea mjini Dodoma. Anaandika Pendo Omary … (endelea).

Akiongea jijini Dar es Saam, John Mnyika, naibu katibu mkuu wa chama hicho, Tanzania Bara, ametaja miswada ambayo chama chake inataka wabunge wa UKAWA kuikwamisha, ni muswada wa Sheria ya Miamala ya Kielektroniki wa mwaka 2014 (The Electronic Transaction Bill, 2015) na muswada wa Sheria ya Makosa ya Mtandao wa mwaka 2015 (The Coputer and Cyber Crimes Bill, 2015).

Miswada mingine, ni Muswada wa Sheria ya Kupata Habari wa mwaka 2015 (The Acces to Information Bill, 2015) na Muswada wa Sheria ya Vyombo vya Habari wa Mwaka 2015 (The Media Services Bill, 2015).

Muswada wa Sheria ya miamala ya kielektroniki na muswada wa sheria ya makosa ya mtandao, inatarajiwa kuwasilishwa bungeni kwa hati ya dharura, tarehe 26 Machi mwaka huu.

Muswada wa Sheria ya kupata habari na ule wa vyombo vya habari, umepangwa kusomwa kwa mara ya kwanza na hatua zake zote ikiwemo kupitishwa kwa hati ya dharura, tarehe 27 Machi mwaka huu.

Mnyika amesema vipo viashiria vingi vinavyoonesha serikali haina nia nzuri ya kupeleka miswada hiyo bungeni. “Kati ya mwaka 2007-2008 serikali ilipokea muswada wa wadau wa habari. Lakini sasa, serikali imeitupa maoni yake na kuleta muswada mpya ambao hauna maoni ya wadau.”

Mnyika amesema serikali haiaminiki. Inatuhumiwa kutumia vyombo vya dola kudhuru wanahabari na kuvifungia vyombo vya habari; inataka kupeleka miswada hiyo kwa hati ya dharura kwa kuwa inataka kuvifungia vyombo hivyo.

“Baada ya kufungiwa kwa gazeti la MwanaHALISI kwa muda usio julikana, Kubenea (Saed Kubenea), amefungua mtandao wa MwanaHALISI Online. Huu ndiyo mtandao ambao hauogopi katika kutoa taarifa, Lengo la muswada huu ni kuvibana vyombo huru vya habari kama huu mtandao,” amesisitiza.

Aidha Mnyika amesema “miswada hiyo inahitaji mjadala wa kitaifa, “mpaka sasa wabunge hawajapewa miswada hiyo.”

error: Content is protected !!