September 25, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Chadema: Maandalizi UKUTA yanoga

Spread the love

UONGOZI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wamesema, maandalizi ya mikutano ya UKUTA katika Mkoa wa Dodoma yamefikia hatua nzuri, anaandika Dany Tibason.

Pia uongozi huo wamelaani Jeshi la Polisi kukamata na kuwasababishia usumbufu wanachama wa chama hicho hususan wanavyuo.

Jella Mambo, Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Dodoma ametoa tamko hilo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi ya chama hicho Kanda ya Kati.

Mambo amesema, Chadema Mkoa wa Dodoma wanaunga mkono tamko la viongo wa kitaifa juu ya ufanyaji wa mikutano na maandamano kwa lengo la kukabiliana uvunjifu wa katiba unaofanywa na watawala.

Amesema, mbali na kuwa maadalizi ya ufanywaji wa mikutano na maandamano kukamilika pia wanalaani tabia ya matamkoa ambayo yanatolewa na viongozi wa juu wa serikali kwa kuwatishia baadhi ya wananchi kwamba kufanyika kwa mikutano na maandamano ni dalili za uvunjifu wa amani.

“Yapo matamko ya viongozi wa juu serikalini yakiwa yanalenga kuwatishia wananchi au kuwadhalilisha viongozi wa juu katika vyama vya upinzani.

“Pamoja na kuwepo kwa kauli za ubabe zinazotolewa na viongizi wa serikali, bado sisi viongozi na wanachama wa Chadema hatutaweza kurudi nyuma hata kidogo.

“Kutokana na hali hiyo tunaendelea kuwahamasisha vijana ambao ni wanachama pamoja na wale wenye kutaka haki wajitokeze siku ya Septemba Mosi,” amesisitiza Mambo.

Kuhusu Jeshi la Polisi amesema, wamekuwa mstari wa mbele zaidi katika kuvunja Katiba ya nchi kwa kuzuia mikutano ya kisiasa kwa kisingizio kuwa, wanapata maelekezo kutoka juu.

Amesema, mikutano na maandamano ipo kisheria na ni wajibu wa vyama vya siasa kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi na siyo kuomba kibali.

error: Content is protected !!