Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Chadema kwenda na majeruhi wa risasi kortini
Habari za Siasa

Chadema kwenda na majeruhi wa risasi kortini

Viongozi wa Chadema wakiwa nje ya mahakama ya Kisutu baada ya kesi yao inayowakabiri
Spread the love

UPANDE utetezi kwenye kesi ya uchochezi namba 112/2018, inayowakabili viongozi tisa wa Chadema, umepanga kwenda mahakamani na mashahidi waliojeruhiwa kwa risasi. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Hata hivyo, leo tarehe 24 Septemba 2019 upande wa utetezi umeomba ahirisho la kesi hiyo, kutokana na washtakiwa wawili kutokuwepo huku hoja nyingine ikiwa ni kijipanga kwa ushahidi.

Katika kesi hiyo, iliyopo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, Dk. Vincent Mashinji, hakuwepo mahakamani kutokana na dharura.

Dk. Mashinji na Ester Matiko ambao ni miongoni mwa washtakiwa hao, kupitia wakili wao Prof. Abdallah Safari, wameomba ruhusa ya mahakama kusafiri nje nchi.

Washtakiwa kwenye kesi hiyo ni pamoja na Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema-Taifa; Dk. Mashinji, Katibu Mkuu wa chama hiko; John Mnyika, Naibu Katibu Bara na Salum Mwalimu, Naibu Katibu Zanzibar.

Wengine ni Halima Mdee, Mbunge wa Kawe; Matiko ambaye ni Mbunge wa Tarime Mjini; Ester Bulaya, Mbunge wa Bunda Mjini; John Heche, Mbunge wa Tarime Vijijini na Mchungaji Peter Msigwa, Mbunge wa Iringa Mjini.

Mbali na Prof. Safari, upande wa utetezi umewakilishwa na Peter Kibatala, Hekima Mwasipu, John Mallya na Dickson Matata.

Upande wa serikali umewakilishwa na Faraja Nchimbi, Dk. Zainabu Mchimbi,Wakili wa Serikali Mkuu; Wankyo Simon, Wakili wa Serikali Mwandamizi.

Awali, Profesa Safari amedai, kuwa mshtakiwa Dk. Mashinji amehudhuria kwenye kesi namba 9 ya mwaka 2017 ya uchochezi inayomkabili kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Songea ambayo ilikuwa kwenye hatua ya ukilizwaji.

Amedai, upande wa Jamhuri haukuweka wazi idadi ya mashahidi wala siku yao ya kufunga ushahidi wao, na waliushtukiza upande wa utetezi ilhali wanajua kuna maandalizi ya utetezi.

Prof. Safari ameitaja ibara ya 13 ya Katiba inayoeleza juu ya haki ya kusikilizwa kwa washtakiwa kikamilifu.

Licha ya kuieleza mahakama hiyo kuwa tarehe 26 Septemba hadi tarehe 6 Oktoba 2019, mshtakiwa Mashinji ameiandikia barua kuwa atakuwa safarini Uengereza, upande huo wanao mashahidi waliojeruhiwa kwa risasi ambao wanawaanda kuwaleta mahakamani hapo.

Prof. Safari amedai mahakamani hapo, mshitakiwa  wa tano (Matiko), amealikwa kupitia Ofisi ya Bunge kuanzia tarehe 25 hadi 28 Septemba mwaka huu kwenda Kigali-Rwanda.

Hata Prof. Safari ameeleza kuwa 13 – 18 Septemba Oktoba 2019, mshtakiwa Matiko amealikwa kwenye Bunge la Umoja wa Ulaya kama Mjumbe wa Afrika.

Baada ya kueleza hayo, Prof. Safari ameiomba mahakama kupanga siku ya tarehe 7 na 8 Oktoba mwaka huu kwa ajili ya kuendelea.

Wakili Nchimbi akijibu hoja hizo, ameeleza kwa kuwa wito wa Dk. Mashinji mahakamani unaonekana aliitwa kwenye kesi jana tarehe 23 Septemba 2019, hivyo leo anaweza kuwa njiani na kesho akaja mahakamani kwa ajili ya kuendelea.

Nchimbi ameeleza, kuwa katika barua ya kuomba mahakama ruhusa ya safari ya Dk. Mashinji, haikuainisha anakwenda Uengereza kufanya nini.

Pia Nchimbi ameeleza, dharura ya Matiko ya kwenda Kigali, Rwanda ni ombi linalotoka kwenye Taasisi ya Mawakili Wanawake wa Tanzania (TAWLA), lilowasilishwa kwa katibu wa wabunge, hivyo anaweza kukubaliwa ama kukataliwa na kwamba, wapo wabunge sita, yeye hana ulazima wa kwenda.

Baada ya kusiliza pande zote mbili, Hakimu Simba ameamua kuahirisha shauri hilo mpaka kesho tarehe 25  atakapotoa uamuzi juu ya mabishano hayo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!