March 3, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Chadema kwenda mahakamani kupinga ushindi wa CCM

Nyundo ya Hakimu

Spread the love

CHAMA cha Demorasia na Maendeleo (Chadema), mkoani Mara, kimepanga kwenda mahakamani kupinga ushindi wa mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika uchaguzi mdogo wa udiwani kata ya Turwa, wilayani Tarime. Anaripoti Regina Kelvin … (endelea).

Hayo yameelezwa jana na Katibu wa chama hicho hicho mkoani Mara, Chacha Heche, alipokuwa akizungumza na wandishi wa habari, wilayani Tarime.

Heche alidai kuwa Msimamizi Msaidizi wa uchaguzi huo mdogo kata ya Turwa, Peter Julius, alikiuka baadhi ya taratibu za sheria ya uchaguzi, ikiwemo mawakala wa Chadema kutokabidhiwa fomu Na. 21c na 24c pamoja na matokeo yake.

Amesema, “…huyu bwana amevuruga uchaguzi huu, kwa makusudi. Kwa makusudi, amekiuka kwa makusudi, sheria na kanuni za uchaguzi kwa maslahi ya CCM na mawakala wake.”

Naye aliyekuwa mgombea udiwani wa kata hiyo kupitia Chadema, Charles Mnanka, alidai kuwa atakwenda mahakamani kupinga matokeo ya uchaguzi huo yaliyompa ushindi Chacha Ghati kutokana na kuwapo ukiukwaji wa sheria.

Mnanka alimtuhumu msimamizi wa uchaguzi – Peter Julius – kutangaza matokeo ya uchaguzi kwa kukipendelea CCM; na kuongeza kuwa “Chadema kilipata kura nyingi zaidi kuliko CCM, lakini hakikutangazwa mshindi.”

Uchaguzi mdogo katika kata ya Turwa uliofanyika tarehe 12 Agosti mwaka huu, ulitawaliwa na vurugu, vitisho na ukiukwaji mkubwa wa taratibu.

error: Content is protected !!