May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Chadema kuwafikisha kortini OCD Dodoma, Kigoma

Benson Kigaila, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema

Spread the love

 

CHAMA kikuu cha upinzani nchini Tanzania cha Chadema, kimepanga kiwafikisha mahakamani kwa majina yao, Mkuu wa Polisi wa Wilaya (OCD) wa Dodoma Mjini na Kigoma Mjini ili kujibu tuhuma zinazowakabili. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Hilo limesemwa leo Jumamosi, tarehe 7 Agosti 2021 na Benson Kigaila, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, wakati akizungumza na waandishi wa habari, makao makuu ya chama hicho Kinondoni mkoani Dar es Salaam kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo mwenendo wa jeshi la polisi.

Kigaila amesema, kijiwe cha Chadema cha Kigoma kimevunjwa na jeshi la polisi “kwa kutumia gari la polisi la washwashwa.”

“Hatujajua kwa nini wameamua kufanya hivyo na kwa hatua hiyo tumeelekeza mawakili wetu kumfikisha mahakamani OCD wa Kigoma Mjini kwa jina lake mwenyewe. Hatutamfungulia kwa cheo chake bali jina lake yeye kama yeye,” amesema Kigaila

Pia, Kigaila amesema, tarehe 2 Agosti 2021 “jeshi la polisi lilivunja ofisi yetu ya Kanda ya Kati na kuchukua walivyochukua. Hii haikubaliki hata kidogo na tumeelekeza mawakili wetu naye kumfungulia mashtaka OCD wa Dodoma Mjini kwa jina lake.”

“Hii itasaidia ili kama atakutwa na hatia alipe yeye kama yeye siyo cheo chake. Unaweza kujiuliza kwa nini polisi wanakwenda kuvunja ofisi yetu, kwa lengo gani,” amehoji Kigaila

error: Content is protected !!