Sunday , 19 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Chadema kumuenzi Tambwe Hiza kwa ushindi Kinondoni
Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumuenzi Tambwe Hiza kwa ushindi Kinondoni

Spread the love

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeahidi kumuenzi mwanachama wake Richard Tambwe Hiza kwa kushinda na kutangazwa washindi katika jimbo la Kinondoni. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Tambwe Hiza aliyefariki Alfajiri ya Alhamisi, alikuwa Mratibu wa Kampeni wa Jimbo la Kinondoni, ambapo mgombea wake ni Salum Mwalimu.

Ahadi hiyo imetolewa na Makamu Mwenyekiti wa Kanda ya Pwani na Meneja wa Kampeni jimbo la Kinondoni, Saed Kubenea, alipokuwa anatoa salamu za rambirambi katika misa ya kumuaga Marahemu Tambwe Hiza.

Kubenea ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Ubungo, amesema marehemu ameacha pengo kubwa katika chama hasa kwenye kampeni za ubunge jimbo la Kinondoni ambapo siku moja kabla ya kifo chake alikuwa jukwaani kumnadi mgombea wao.

“Tambwe (Hiza) ametuacha wakati tukiwa tunamuhitaji sana katika kampeni. Hakuna cha kusema, lakini tunamuahidi tutamuenzi kwa kushinda uchaguzi na kuhakikisha tunatangazwa washindi katika jimbo la Kinondoni,” amesema Kubenea.

Mazishi ya mwanasiasa huyo yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka vyama vinavyounda umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) akiwemo Edward Lowassa mjumbe wa Kamati Kuu Chadema, Abdallah Safari, Makamo Mwenyekiti wa Chadema na Vicent Mashinji, Katibu Mkuu wa Chadema.

Abdallah Mtolea, Mbunge wa Temeke, Godbless Lema, Mbunge wa Arusha na wafausi wengine wa chama hicho.

Kwa upande wake, Lowassa amesema anamfahamu vizuri marehemu jinsi alivyokuwa na msimamo wa kisiasa, hivyo chama chake kimepoteza mtu muhimu sana.

Katibu wa Chadema, Mashinji amesema Tambwe Hiza ameondoka huku akiwa anasuburi kampeni za Kinondlni ziiishe ili amkabidhi kitengo cha Propaganga, lakini kabla hayo hayajatimia Mungu amemchukua.

Naye Lema aliwatia matumaini watoto wa marehemu na mke wake, kuwa wanaweza kuishi bila kuwepo kwa mzazi wao, kikubwa ni kumwamini Mungu kwani yeye ndiyo mlezi wa wote.

Mchungaji Peter Msigwa ameeleza kuwa Hiza ameishi kwa muda mfupi lakini maisha yake yalikuwa na tija kwa Taifa, kwani kuna watu wanaishi miaka mingi lakini hawana lolote walilofanya.

 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

CCM yamteua Pele kuwa mgombea ubunge Kwahani

Spread the loveKamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Ujenzi kituo cha kupoza umeme Chalinze wafikia asilimia 93.7

Spread the loveKamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imeeleza...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Wakili Mwabukusi anusurika kufungiwa, asema hatarudi nyuma

Spread the loveWAKILI Boniface Mwabukusi amesema kuwa hatorudi nyuma kuwatetea Watanzania na...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

RC Chongolo atangaza ‘vita’ kwa wanaovusha wageni kinyemela

Spread the loveKATIKA kulinda usalama wa nchi kupitia mpaka wa Songwe, Mkuu...

error: Content is protected !!