Thursday , 25 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Chadema kumlalamikia Rais Samia mahakamani
Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumlalamikia Rais Samia mahakamani

John Mnyika, Katibu Mkuu wa Chadema
Spread the love

 

CHAMA kikuu cha upinzani nchini Tanzania cha Chadema, kimedai kauli ya Rais Samia Suluhu Hassan, dhidi ya mashtaka ya kula njama za ugaidi yanayomkabili kiongozi wa chama hicho, Freeman Mbowe na wenzake watatu, imeingilia uhuru wa mahakama. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Kauli hiyo imetolewa leo Jumanne, tarehe 10 Agosti 2021 na Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika, wakati akizungumza na waandishi wa habari, makao makuu ya chama hicho, Kinondoni mkoani Dar es Salaam.

Lengo la kukutana na waandishi wa habari ni kuzungumzia mahojiano aliyofanyiwa Rais Samia jana Jumatatu na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), Ikulu ya Dar es Salaam.

Katika mahojiano hayo, Rais Samia alisema aliulizwa swali la mtangazaji wa BBC, Salim Kikeke juu ya kukamatwa na kufunguliwa kesi ya ugaidi Mbowe kuwa imechochewa na harakati za kisiasa.

Akijibu swali hilo, Rais Samia alisema “kama utakumbuka Mbowe kipindi kirefu hakuwepo nchini, alikuwepo Nairobi. Kwa nini kakimbia sijui, lakini alivyoingia tu nchini kaitisha maandamano ya madai ya katiba, nadhani ni mahesabu, amejua kwamba ana kesi ya aina hiyo na hii vurugu akikamatwa aseme kwa sababu ya katiba.”

Rais Samia Suluhu Hassan

Hata hivyo, Mnyika amesema “kauli ya Rais aliyoitoa jana kuhusu Mbowe, ni jambo kubwa katika Taifa, ambalo kwa misingi ya kidemokrasia kunapaswa kuwe na uhuru wa mihimili. Kuingilia uhuru wa mahakama na mwenendo wa shauri hakupaswi kuachwa bila kutolewa kauli na hatua kuchukuliwa.”

Mnyika amesema, Chadema kitatumia njia za kisheria kupinga kauli hiyo ya Rais Samia, kuhusu mashtaka yanayomkabili Mbowe na wenzake, kwenye kesi ya uhujumu uchumi Na. 63/2020, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam.

Mtendaji mkuu huyo wa Chadema amesema, tayari chama hicho kimewaelekeza mawakili wanaosimamia kesi hiyo wakiongozwa na Peter Kibatala wachukue hatua dhidi ya kauli hizo.

“Kufuatia mahojiano hayo ya Rais, katika maeneo yote aliyozungumza dhidi ya Mbowe yenye muelekeo wa kuingilia shauri mahakamani na mahakama, tayari chama kimetoa maelekezo kwa jopo la mawakili wa chama wanaosimamia kesi ya Mbowe, kuweza kuchukua hatua juu ya kauli zilizotolewa na Rais kwa kutumia njia za kimahakama,” amesema Mnyika.

Aidha, Mnyika amesema Mbowe hakukimbia nchi kama ilivyoelezwa na Rais Samia na wala hakushtakiwa kwa makosa hayo Septemba 2020, kama kiongozi huyo alivyosema.

“Mwenyekiti kwa kuwa hakushtakiwa mahakamani hiyo Septemba 2020 kama anavyodai Rais, hakuna wakati wowote eti amekimbia nchi kwa sababu alijua ana shauri linalomkabili mahakamani. Jambo hili si kweli, umma wa Watanzania na jumuiya za kimataifa ipuuze kauli hizi zilizotolewa na Rais,” amesema Mnyika.

Mnyika amesema “na katika wakati muafaka, katika njia za kimahakama tutaeleza kiundani juu ya safari za Mbowe na kazi alizofanya. Wakati gani alikuwa Tanzania, alitoka Tanzania kwa njia zipi. Mbowe alitoka kihalali kabisa, bila kutoroka. Hakutafutwa wakati wowote, haya yatabainika jambo hili litakapokwenda kwenye mahakama na kushughulikiwa kwa njia za kimahakama.”

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema

Mwanasiasa huyo amesema, Mbowe alifunguliwa rasmi kesi hiyo tarehe 26 Julai 2021, kisha kusomewa upya mashtaka hayo tarehe 5 Agosti 2021, baada ya kuunganishwa na wenzake watatu, waliofikishwa mahakamani tarehe 19 Agosti mwaka jana.

“Rais wa Tanzania amedai mwenyekiti Mbowe na wenzake walifunguliwa kesi mwezi Septemba mwaka jana, kauli hii ya Rais ni ya uongo ni ama Rais amepotoshwa na watu wake au ameamua kusema uongo. Hakuna kesi yoyote ya ugaidi au uhujumu uchumi ambayo Mbowe alifunguliwa Septemba 2020,” amesema Mnyika.

“Kwa mara ya kwanza kabisa Mbowe amefunguliwa kesi mahakamani tarehe 26 Julai 2021, siku chache zilizopita, mwenyekiti hakuwahi kuwa na kesi ya namna hiyo iliyozungumzwa na Rais, jamii ya kimataifa itambue kauli ya Rais ni ya uongo,” amesema

Mbali na Mbowe, washtakiwa wengine kwenye kesi hiyo ni, Halfan Bwire Hassan, Adam Hassan Kasekwa na Mohammed Abdillah Lingwenya.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

error: Content is protected !!