July 28, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Chadema kumjadili Magufuli

Spread the love

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kinatarajia kujadili mwenendo wa utawala wa Rais John Magufuli, anaandika Pendo Omary.

Taarifa iliyotolewa mchana huu kwa vyombo vya habari na Tumaini Makene, Afisa Habari wa Chadema inasema Kamati Kuu ya Chama itakutana Mjini Dodoma katika kikao chake cha kikatiba kuanzia Mei 12-1.

“Pamoja na masuala mengine, kitajadili kwa kina taarifa ya hali ya siasa nchini Sambamba na mwenendo wa Serikali ya CCM ya awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli ambayo imetimiza miezi 6 madarakani,” inasema sehemu ya taarifa hiyo.

Aidha, kikao hicho, kitajadili na kupitisha mpango kazi wa chama hicho kwa mwaka huu ambao unatokana na mpango mkakati wa chama wa miaka mitano.

“Kabla ya Sekretarieti kuanza utekelezaji, ambao utahusisha shughuli mbalimbali za chama ikiwa ni pamoja na uimarishaji wa chama nchi nzima na kuendelea kuwatumikia wananchi,” imesema taarifa hiyo.

error: Content is protected !!