Thursday , 23 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Chadema kukutana kwa dharura kumtafuta Mbowe, yamwomba Rais Samia…
Habari za SiasaTangulizi

Chadema kukutana kwa dharura kumtafuta Mbowe, yamwomba Rais Samia…

Spread the love

 

CHAMA kikuu cha upinzani nchini Tanzania-Chadema, kimeitisha kikao cha dharura cha kamati kuu, kwa ajili ya kumtafuta mwenyekiti wao, Freeman Mbowe, ambaye hajulikani alipo. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea). 

Mbowe anadaiwa kukamatwa na wenzake 11 saa 8 usiku wa kuamkia leo Jumatano, tarehe 21 Julai 2021, katika Hotel ya Kingdom jijini Mwanza na jeshi la polisi.

Hata hivyo, taarifa iliyotolewa leo asubuhi na Chadema, imeeleza viongizi hao 11 akiwemo mwanazuioni Dk. Azaveli Lwaitama, wapo kituo kikuu cha polisi Mwanza huku Mbowe akiwa hajulikani alipo.

Tangu kutokea kwa tukio hilo, Jeshi la Polisi, halijatoa taarifa yoyote ya ama Mbowe inamshikilia au la pamoja ma hao 11.

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema

Mbowe na wenzake 11, wamekamatwa ikiwa ni saa chache zilikuwa zimebaki kabla ya kufanyika kwa kingamano la kudai Katiba mpya, mkoani humo.

Kufuatia tukio hilo, Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika, amekutana na waandishi wa habari, makao makuu ya chama hicho, Kinondoni mkoani Dar es Salam akisema, kikao hicho cha dharura cha kamati kuu kitafanyika kesho Alhamisi tarehe 22 Julai 2021, na kwamba baada ya kufanyika chama hicho kitatoa maazimio.

“Kwa upande wetu tumeitisha kikao cha dharura cha kamati kuu ya chama, kitafanyika kesho tutaendelea kumtafuta leo na siku ya kesho. Baada ya kikao tutaueleza umma wa Watanzania hatua za ziada tutakazochukua,” amesema Mnyika. Hakueleza kikao hicho kitafanyika wapi.

Wakati huo huo, Mnyika amewaomba viongozi na wanachama wa Chadema nchi nzima wapaze sauti zao kumtafuta Mbowe.

“Niwaelekeze viongozi na wanachama nchi nzima, sababu mbowe hajulikani yuko wapi na ana  hali gani, kuanzia muda huu ninapozungumza kazi ya kumtafuta mwenyekiti iendelee nchi nzima,” amesema Mnyika.

“Haijulikani Mbowe yuko wapi na ana hali gani, taarifa kutoka vyombo vyetu ndani ya Jeshi la  Polisi zinasema ameondolewa ndani ya Mkoa wa Mwanza na haieleweki amepelekwa mkoa gani.”

“Mbowe ndiye kiongozi wetu mkuu wa chama kwa kitendo hiki kiongozi kuchukuliwa kinyume cha sheria kupelekwa kusikojulikana kwa hali ilipofikia sasa jambo hili tunalipeleka kwa wanachama wetu ili tuweze kushirikiana kwa pamoja,” amesema Mnyika.

Aidha, Mnyika amemuomba Rais Samia Suluhu Hassan, aingilie kati kuhusu tukio hilo, ikiwemo kuagiza vyombo vya dola kumuacha huru Mbowe na wenzake.

“Tunamuomba Rais Samia aagize vyombo vyake vya ulinzi na usalama vimuachie Freeman Mbowe na wengine 11 waliokamatwa usiku wa kuamkia leo Mwanza wakiwa katika maandalizi ya kongamano la kudai katiba mpya,” amesema Mnyika.

Kongamano hilo liliandaliwa na Bavicha, ambapo limeshazuiwa mara mbili kufanyika. Mara ya kwanza lilipangwa kufanyika tarehe 17 Julai 2021, lakini Jeshi la Polisi lilizuia kwa madai ya kukosa kibali.

Mara ya pili lilipangwa kufanyika leo, lakini limezuiwa kwa maelekezo ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Robert Gabriel, aliyepiga marufuku mikusanyiko kwa malezo ya kudhibiti maambukizi ya ugonjwa wa Covid-19.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia aagiza iundwe kamati ya pamoja ya Mawaziri mradi wa BBT

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amewaagiza mawaziri kuunda kamati...

Habari za Siasa

Rais Samia apangua makatibu tawala mikoa, ateua Kamishna DCEA

Spread the loveALIYEKUWA Kamishna wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya, Gerald...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

M/kiti bodi ya wadhamini Chadema afariki dunia

Spread the loveMWENYEKITI wa Bodi ya Wadhamini ya Chama cha Demokrasia na...

Habari za Siasa

Zitto: Nikifa Ado atavaa viatu vyangu

Spread the love  KIONGOZI Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe...

error: Content is protected !!