Wednesday , 6 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Chadema kifua mbele Tunduma, serikali yasusa
Habari za SiasaTangulizi

Chadema kifua mbele Tunduma, serikali yasusa

Ofisi ya Chadema Wilaya ya Tunduma
Spread the love

UJENZI wa barabara, ujenzi wa vyoo, shule na uchimbaji visima umeimarisha taswira ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) katika Halmashauri ya Mji wa Tunduma, Mbeya. Anaripoti Ibrahim Yassin … (endelea).

“Kuwepo kwa mabadiliko makubwa katika sekta mbalimbali ikiwemo ujenzi wa visima vya maji, barabara kuwekwa lami pia ujenzi wa madarasa, kumeendeeleza taswira chanya ya Chadema,” anasema Ally Mwafongo ambaye ni mwenyekiti wa halmashauri hiyo na kuongeza;

“Tumejenga shule mpya nne zilizoshirikisha nguvu za wananchi wakishirikiana na wenyeviti wa serikali za mitaa. Shule hizo tulizipaua na kuongeza ujenzi wa vyoo pamoja na kufanya maboresho.”

Amesema, halmashauri hiyo chini ya uongozi wake wamepanga kuweka lami kwenye barabara tatu ikiwemo ile ya kutoka CCM hadi barabara kuu kilometa 2.5.

“Barabara nyingine ni ya kutoka Transformer hadi Songea na nyingine kutoka eneo la matuta barabara kuu kwenda kwenye soko la jioni (Mbambila) na tayari mifereji ilichimba na kuanza hatua za awali, imebakia kuwekwa lami ambayo ina mita 700.

“Zitazofuata ni ile ya kutoka Maporomoko hadi Ihanda kilometa 1 na Kilimanjaro hadi Tazara yenye Kilometa 1,” amesema Mwafongo.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mlimani uliyopo kwenye Kata ya Maporomoko, Joseph Mwachembe (China) amesema, Chadema inatengwa na watumishi wa Halmashauri ya Mji wa Tunduma.

Mwachembe ambaye pia ni Mwenyekiti wa Mkoa wa Mbeya wa chama hicho anasema, watendaji wa halmashauri ya mji huo aidha wamepewa maelekezo ama wameamua kugoma kufanya kazi na wenyeviti 45 wa Chadema bila kuelezwa sababu za msingi.

“Sisi tunahujumiwa, kila tunapofanya jambo watendaji wa halmashauri wanajitenga, tupo kwenye mikakati ya kumuandikia barua mkurugenzi wao ili tujue kosa letu.

“Naamini tunafanyiwa vitendo hivyo kwasababu tu kata hizo zinaongozwa na wenyeviti pia diwani wa Chadema. Hi si haki,’’anasema.

Anasema, walipoingia madarakani wananchi waliwachagua madiwani 14 wa Chadema kwenye Kati ya 15 za mji huo ambapo waliwapa nafasi ya Viti Maalum vitano na kufanya jumla yao kuwa 20 huku CCM ikipata diwani mmoja na kufanya idadi yao kwenye Baraza la Madiwani kuwa 21. Madiwani watatu wamekimbilia CCM.

Mwachembe amesema, walipoingia madarakani walikuta makisio ya makusanyo ya Sh. bilion 1.8 yaliyopangwa, iliyoachwa na mwenyekiti wa mamlaka ya mji mdogo wa serikali za mitaa kabla yao, EliasCheyo (CCM) aliyeongoza mwaka 2009 hadi 2014.

Na kwamba, baada ya mwenyekiti huyo kuondoka, Salvatory Ngole wa CHADEMA aliongoza kwa miezi sita na baada ya hapo, mwaka 2015 aliingia mwenyekiti mpya wa Halmashauri ya Mji, Ally Mwafongo (CHADEMA) ambao waliikuta hati chafu na kuanza mikakati mipya.

“Kilichofanywa na mwenyekiti mpya kwanza ilikuwa kuhakikisha anaziba mianya yote ya ukwapuaji iliyokuwa inatumiwa na viongozi wa Halmashauri pia CCM,” anasema Mwachembe.

Anasema, maeoneo yaliyoshughulikiwa kwa karibu zaidi ni utoroshaji wa mapato ambao kwa kiasi kikubwa ulisababisha halmashauri hiyo kupata hati chafu.

Na baada ya hapo anasema, makadirio ya bajeti yaliongezeka na kufikia bajeti ya Sh. bilioni 4.2 kwa mwaka 2017/18 huku malengu makuu yakielekezwa kwenye elimu, afya, maji, miundombinu ikiwemo ununuzi wa magari madogo ya ofisi na yale ya kuzolea taka baada ya halmashauri hiyo kutokuwa na magari kwa kuwa ni mpya.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Bashungwa: Katesh kutafanyiwa usafi wa hali ya juu

Spread the loveWAZIRI wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amesema kazi ya kuondoa tope...

AfyaHabari za Siasa

RAS Songwe: Tumepigwa… mkurugenzi nakupa siku 21

Spread the loveKATIBU tawala mkoani Songwe, Happines Seneda ametoa siku 21 kwa...

BiasharaTangulizi

Bei ya Dizeli, Petroli yashuka

Spread the loveBEI ya mafuta kwa mwezi Disemba, imeshuka kutokana na kupungua...

Habari za Siasa

Dk. Biteko: Viongozi tuache alama nzuri katika utendaji wetu

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!