August 17, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Chadema kanda ya kati yatangaza mapambano

Tundu Lissu, Mbunge wa Singida Mashariki

Spread the love

UONGOZI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kanda ya kati umetangaza kuingia katika mapambano ya kukiimarisha chama hicho katika mikoa ya kanda hiyo, anaandika Dany Tibason.

Kanda ya kati ni miongoni mwa kanda kumi za Chadema ambazo zinaendelea na uchaguzi wa kupata viongozi wake wapya.

Alphonce Mbassah, mwenyekiti wa Chadema kanda ya kati ameiambia MwanaHALISI Online katika mahojiano maalum kuwa wanayo mipango kabambe ya kukiimarisha chama hicho katika mikoa ya Morogoro, Singida na Dodoma ili kufanya vizuri katika chaguzi zijazo.

“Uchaguzi umemalizika kilichobaki kwa sasa ni kufanya kazi ya kukijenga chama pamoja na kuimarisha uongozi wa chama katika kanda ya kati sambamba na kuwajengea uwezo wanachama, kuwatia ujasiri na kupanga mipango ya ushindi,” amesema.

Akizungumzia kitendo cha Kamati Kuu ya Chadema kuuvunja uongozi wa mkoa wa Dodoma, amesema jambo hilo haliwezi kupingwa na mtu yoyote bali kinachotakiwa ni kufanya kazi ambayo inalenga kujenga chama.

“Kwa sasa kanda ina uongozi na kwa maana hiyo tunajipanga kuhakikisha chama kinaimarika na viongozi waliopo wanafanya kazi ya kujenga chama, tunaheshimu mamlaka na maamuzi ya Kamati Kuu yetu,” amesisitiza na kuongeza;

“Kanda yetu ina jumla ya kata 559, majimbo 29 katika mikoa mitatu lakini Chadema tunashikilia majimbo manne tu. Ni lazima tujipange vizuri ili kuing’oa CCM ambayo imeweka ngome yake katika kanda hii.”

error: Content is protected !!