June 16, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Chadema: JPM anachukia pombe kuliko ufisadi?

Spread the love

HATUA ya Rais John Pombe Magufuli kumtimua kazi Charles Kitwanga, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi imeibua maswali,” anaandika Pendo Omary.

Miongoni mwa maswali hayo ni pamoja na kwamba, Rais Magufuli anachukia zaidi pombe kuliko ufisadi? Ni kwa madai hukumu ya pombe imepewa kipaumbe zaidi juu ya mtuhumiwa zaidi ya harufu ya ufisadi anaotuhumiwa nao.

Swali hilo limehojiwa na Julius Mwita, Katibu Mkuu Baraza la Vijana (Bavicha) baada ya kuzungumza na Mwanahalisi Online leo jijini Dar es Salaam. “Rais anachukia pombe kuliko ufisadi?” amehoji.

Mwita amedai kuwa, hatua ya Rais Magufuli kutengua uteuzi wa Kitwanga ni kukwepa mapendekezo yaliyotolewa na baraza hilo.

Mapendekezo hayo ni kuhusu kumchukulia hatua Kitwanga ili kupisha uchunguzi wa mkataba tata ulioingiwa kati ya Kampuni ya Lugumi na Jeshi la Polisi.

Katika taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana jioni na Gerson Msigwa, Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, Ikulu imeeleza kuwa “Rais Magufuli ametengua uteuzi huo kufuatia kitendo cha Mheshimiwa Charles Kitwanga kuingia bungeni na kujibu swali linalohusu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi akiwa amelewa.”

Mwita amesema “tulitaka Rais Magufuli kutengua uteuzi wa Charles Kitwanga au Kitwanga ajiuzulu mwenyewe ili kupisha uchunguzi wa mkataba tata baina ya Jeshi la Polisi na Kampuni ya Lugumi Enterprises.

“Hii ingetoa uhuru kwa kamati ndogo ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kufuatilia suala hili kwa undani. Alichokifanya Magufuli ni kuwaziba watu macho. Je, Magufuli anachukia zaidi ulevi kuliko ufisadi,” amesema Mwita.

Mwita amesema, uchunguzi utakaofanywa na kamati ndogo ya PAC unapaswa kuwekwa hadharani na kujulikana kwa Watanzania wote ili waujadili.

“Baada ya uchunguzi huo. Watu wote waliotajwa wanapaswa kuchukuliwa hatua zaidi. Rais Magufuli aliahidi kufungua Mahakama ya Mafisadi, anapaswa kutimiza ahadi yake,” amesema Mwita.

error: Content is protected !!