Sunday , 2 April 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Chadema: Hatumchukii Magufuli, ila…
Habari za Siasa

Chadema: Hatumchukii Magufuli, ila…

Spread the love

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), nchini Tanzania, kimeeleza hakina tatizo na Rais John Magufuli, mgombea urais wa nchi hiyo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) bali sera zake. Anaripoti Regina Mkonde…(endelea).

“Hatuna kinyongo na Rais Magufuli, awe na amani, hatuna ugomvi naye, tuna ugomvi na sera zake, ndio maana tumemwambia akae pembeni,” ni kauli ya Salum Mwalimu, mgombea mwenza wa urais wa Tanzania kupitia chama hicho aliyoitoa jana tarehe 17 Septemba 2020 wakati akizungumza kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika Kata ya Ikungi, Singida.

Hata hivyo, chama hicho kimeahidi kumtunza na kumpa heshima Rais Magufuli pindi atakapotoka madarakani. Magufuli aliingia madarakani tarehe 5 Novemba 2015.

“Ninamhakikishia Rais Magufuli, tutamtunza kwa heshima na adabu kama rais mstaafu, tunamwambia akichagua kukaa Chato atakaa kwa amani, akikaa Dar es Salaam atakaa kwa Amani. Tutamchukulia kama rais mstaafu,” amesema Mwalimu.

Amesema, kama Lissu (Tundu Lissu, mgombea urais kupitia Chadema) atashinda katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika tarehe 28 Oktoba 2020, serikali yake haitalipa kisasi kwa mtu yeyote.

“Kwa hiyo niseme, kisasi ni mpango wa Mungu, serikali ya Lissu haikusudii wala haitakusudia kulipa kisasi kwa yoyote na tunataka tumhakikishie, nataka nimhakikishie kama makamu wa rais ajae, tutamtunza vyema kwa heshima na adabu,” amesema Mwalimu

“Serikali yetu tumesema, hatukusudii kulipa kisasi sababu hata waliotuonea hawatuonei kwa kupenda, wanalazimika kufanya hivyo kwa maelekezo kutoka juu, na wao wana watoto wanahitaji maisha bora, hatukusudii kulipa kisasi kwa Rais Magufuli wala serikali yake,” amesema Mwalimu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia apangua mawaziri

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan, amefanya mabadiliko madogo ya Baraza la...

Habari za Siasa

RC mstaafu afariki dunia, CCM yamlilia

Spread the loveALIYEWAHI kuwa mkuu wa mikoa ya Dodoma, Mara, Mtwara na...

Habari za Siasa

Marekani kuwekeza Dola 500 Mil kupeleka bidhaa na huduma Tanzania

Spread the loveMAKAMU wa Rais wa Marekani, Kamala Harris amesema miongoni mwa...

Habari za Siasa

Kamala ataja hatua mpya kuimarisha uhusiano wa kibiashara Tanzania, Marekani

Spread the loveKATIKA kuimaridha uhusiano wa kibiashara na kiuchumi baina ya Tanzania...

error: Content is protected !!