Saturday , 25 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Chadema, CCM watangwana makonde Umeya Dar
Habari za SiasaTangulizi

Chadema, CCM watangwana makonde Umeya Dar

Omary Kumbilamoto, Aliyekuwa Naibu Meya Ilala
Spread the love

MADIWANI wa vyama viwili, Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wale Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wamezichapa wakati wa uchaguzi wa Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, Jijini Dar es Salaam leo tarehe 3 Oktoba 2018. Anaripoti Faki Sosi…(endelea).

Chadema ndio waliokuwa wakija juu zaidi baada ya kuwatuhumu CCM kuiba kura za upinzani kwenye uchaguzi huo uliofanyika katika Ukumbi wa Anatoglou ambapo Diwani wa Kata ya Vingunguti, Omar Kumbilamoto (CCM) ametangazwa kushinda.

Omar ambaye awali alikuwa kwenye nafasi hiyo kupitia Chama cha Wananchi (CUF) na baadaye kuhamia CCM na kisha kusimamishwa kugombea udiwani kwenye uchaguzi mdogo wa marudio uliofanyika hivi karibuni, alitangazwa mshindi wa unaibu meya wa Ilala kwa kupata kura 27 ambapo Adam Rajabu (CUF) alipata kura 25 huku mwakilishi wa Chadema Patrick Assenga akitoka kapa (0).

Kitimtimu kilianza pale uchaguzi ulipomalizika na kura kubebwa kisha kupelekwa kwenye chumba cha kuhesabia kura, Patrick (Chadema) alianza kupiga yowe akituhumu mikakati ya CCM aliyodai kuanza kuvuruga uchaguzi kwa kuiba kura.

Patrick alipiga kelele akidai Rajab alikuwa amebeba kura zake ambazo zilikuwa 27 ambapo polisi walimvaa na kumwamuru arudishe kura hizo na kwamba, matokeo yakapinduliwa kwa kura za CUF zikapelekwa CCM na zile za CCM zikadaiwa kuwa ndio za CUF.

Wakala wa Kumbilamoto alitoka akishangilia kwamba, mgombea wake (Omar) ameibuka mshindi kwenye uchaguzi huo. Kitendo hicho kiliwaghadhibisha madiwani wa upinzani na hapo ulianza ugomvi kwa kupigana ngumi kati ya madiwani wa Chadema, CUF na wale wa CCM huku matusi yakiwatoka madiwani wa upinzani. Hali hiyo ilisababisha polisi kuingilia kati na kutuliza ghasia.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia aagiza iundwe kamati ya pamoja ya Mawaziri mradi wa BBT

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amewaagiza mawaziri kuunda kamati...

Habari za Siasa

Rais Samia apangua makatibu tawala mikoa, ateua Kamishna DCEA

Spread the loveALIYEKUWA Kamishna wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya, Gerald...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

M/kiti bodi ya wadhamini Chadema afariki dunia

Spread the loveMWENYEKITI wa Bodi ya Wadhamini ya Chama cha Demokrasia na...

Habari za Siasa

Zitto: Nikifa Ado atavaa viatu vyangu

Spread the love  KIONGOZI Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe...

error: Content is protected !!