
Biswalo Mganga, aliyekuwa Mkurugenzi wa Mashtaka Tanzania (DPP)
CHAMA Kikuu cha Upizania nchini Tanzania cha Chadema, kimemshauri Rais wa nchi hiyo, Samia Suluhu Hassan, kutomwapisha Biswalo Mganga, kuwa Jaji wa Mahakama Kuu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Chadema wamependekeza, Baraza la Nidhamu limchunguze mwenendo wake alipokuwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) na kama bado anazo sifa za kuteuliwa kuwa Jaji.
Biswalo amehudumu nafasi ya DPP kwa miaka sita na miezi saba, tangu alipoteuliwa tarehe 6 Oktoba 2014 na aliyekuwa Rais wa wakati huo, Jakaya Mrisho Kikwete.
Aliteuliwa kuwa DPP, kuchukua nafasi ya, Dk. Eliezer Feleshi ambaye aliteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu. Sasa Feleshi ni Jaji Kiongozi.
Tangu Biswalo, alipoteuliwa na Rais Samia kuwa Jaji wa Mahakama Kuu, wiki iliyopita, kumekuwa na tuhuma mbalimbali zikitolewa dhidi yake na kushauri mamlaka ya uteuzi kumtengua au kutomwapisha.

Miongoni ni Chadema ambacho kimepinga uteuzi huo na kubainisha njia bora ya kupata majaji wasiokuwa na mgongano wa kimaslahi.
Taarifa ya Chadema, iliyotolewa leo Jumapili, tarehe 16 Mei 2021 na Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa chama hicho, John Mrema imesema, “tunashauri kusitishwa kwa mchakato wa kumuapisha Biswalo kuwa Jaji hadi hapo malalamiko dhidi yake yatakapokamilika.”
Mrema amesmea, mara baada ya malalamiko kukamilika “kuchunguzwa na yatakapoamuliwa na Baraza la Nidhamu (Tribunal) litakaloundwa ili kuchunguza malalamiko na tuhuma dhidi yake.”
Chadema imetoa kauli hiyo, ikiwa imebaki siku moja kabla ya Rais Samia, kesho Jumatatu kuanzia saa 9:00 alasiri, kumwapisha Biswalo na majaji wengine 27, Ikulu ya Dar es Salaam, aliowateua hivi karibuni.
Chama hicho, kimemtuhumu Biswalo kwamba, akiwa DPP alisababisha uwepo wa mahabusu na wafungwa wengi magerezani.

Hata hivyo, MwanaHALISI Online, limemtafuta Biswalo kwa njia ya simu kuhusu tuhuma dhidi yake ikiwemo baadhi kutaka Rais Samia Suluhu Hassan asimwapishe, amesema “siwezi kukujibu chochote kwa mtu ambaye simwoni, kama unahitaji mahojiano na mimi, tuonane uso kwa uso.”
Alipoelezwa wapi anaweza kupatikana alisema, “mtanitafuta nitakapopatikana.”
Kuhusu utaratibu wa kupata majaji, Chadema kimependekeza uwekwe utarataibu wazi wa kuwapata Majaji ikiwa ni pamoja na kuweka wazi uwepo wa nafasi za Ujaji kwa kutangaza ili watu wenye sifa waombe.
“Washindanishwe kwa vigezo na masharti mbalimbali hii ingesaidia kupata Majaji wenye uwezo usiotiliwa shaka, Majaji huru na wasiopendelewa au wasiozua minong’ono ya kubebwa au wenye nasaba za kisiasa,” amesema Mrema.
Ikubaliwe kwamba Biswalo ana tuhuma nyingi sana zikiwemo za kuwataka washtakiwa wa kesi za uhujum uchumi kulipa pesa kupitia account zake binafsi hii si sawa tunamshauri Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mama yetu Samia Suluhu Hassan kutopuuza malalamiko ya wanainchi wake.
Biswalo alipokuwa DPP hakupokea tuu fedha bali hata kuwapa watu kesi zisizo zao mfano mtu anashtakiwa kwa makosa ya kisiasa yeye aliwapa kesi za uhujum uchumi na akajiwekea utaratibu wake kinyume na sheria yenyewe ya uhujum uchumi