Friday , 1 March 2024
Home Kitengo Biashara CEO NMB ashiriki mkutano wa Benki ya Dunia
Biashara

CEO NMB ashiriki mkutano wa Benki ya Dunia

Spread the love

Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna ameshiriki uzinduzi wa Mkutano Mkuu wa Benki ya Dunia (IDA20 Mid Term Review) unaofanyika kwa siku tatu Visiwani Zanzibar. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Huu ni Mkutano wa 20 unaolenga kufanya tathmini ya muda wa kati kupitia Taasisi ya Kimataifa ya Maendeleo ya Benki ya Dunia.

Mkutano huo umefunguliwa leo Jumatano na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Mwinyi na kuhudhuriwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar – Hemed Suleiman Abdalla, Waziri wa Fedha wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mwigulu Nchemba, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania – Emmanuel Tutuba na viongozi wengine.

Akiwa katika mkutano huo, Ruth alipata nafasi pia ya kukutana na Rais wa Benki ya Dunia – Ajaypal Singh Banga.

Benki ya NMB inajivunia kuwa sehemu ya kufanikisha mkutano huu mkubwa Tanzania unaowakutanisha wajumbe zaidi ya 3,000 kutoka mataifa takribani 100 duniani.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Biashara

Expnase yashusha chuma hiki hapa “Super Beli” ndani ya Meridianbet kasino

Spread the love Expanse Studios ina mchezo mpya wa kasino mtandaoniutakaoupenda! Unaitwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Washindi 12 NMB MastaBata na wenza wao wapaa Afrika Kusini

Spread the loveWASHINDI 12 wa kampeni ya kuhamasisha matumizi yasiyohusisha pesa taslimu...

Biashara

Meridianbet yaimarisha usafi Kijitonyama

Spread the loveMABINGWA wa michezo ya kubashiri kampuni ya Meridianbet leo imefanikiwa kufika...

Biashara

Kampeni SBL ya unywaji pombe chini ya umri yafika Kilimanjaro

Spread the loveKAMPUNI ya bia ya Serengeti Breweries Limited (SBL) inewahimiza wanafunzi...

error: Content is protected !!