January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

CDA yaonya uvamizi wa viwanja Dodoma

Spread the love

MAMLAKA ya Ustawishaji Makao Makao Makuu (CDA) imewataka wananchi wanaoendesha kilimo cha mpunga katika viwanja vya makazi ya watu kuondoka mara moja vinginevyo watachukuliwa hatua kali za kisheria. Anaandika Dany Tibason, Dodoma … (endelea).

Kauli hiyo ilitolewa na Kaimu Mkurugenzi wa (CDA), Paskas Muragili alipotembelea maeneo ya Ilazo ambapo kumepimwa kwa ajili ya makazi ya watu lakini kuna baadhi ya wakulima ambao wameanzisha kilimo cha majaluba ya mpunga.

Amesema kitendo cha wakulima kuvamia viwanja vya makazi na kuanzisha kilimo ni uharibifu wa miundombinu ambayo inatengenezwa na Mamlaka hiyo.

Mbali na hilo amesema wakulima hao kwa sasa wamehamisha mkondo wa maji na matokeo yake maji yamesambaa katika nyumba za watu na kusababisha usumbufu mkubwa.

Muragili amesema kutokana na kuwepo kwa wakulima hao wamesababisha kung’oa mambo ambazo uwekwa kama ishara ya mipaka ya viwanja.

Muragili amesema iwapo wakulima hao wasipoyaondoa majaruba yao wenyewe CDA watayasambaratisha wenyewe huku wakulima hao wakipelekwa katika vyombo vya sheria.

Wakati huohuo amewataka wamiliki wa viwanja kuhakikisha wanaendeleza viwanja vyao la sivyo watanyang’anywa na kupewa wengine.

Amesema kwamba wapo watu ambao hawajaendeleza viwanja vyao kwa muda mrefu hivyo viwanja hivyo watapewa watu wengine.

error: Content is protected !!