October 21, 2021

Uhuru hauna Mipaka

CDA yakopa Bil 3.4 kulipa fidia

Spread the love

MAMLAKA ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA), imelazimika kukopa jumla ya Sh. 3.4 bilioni kutoka katika taasisi za kifedha kwa lengo la kulipa fidia wananchi 5500 wa eneo la Mkonze na Mkalama katika Manispaa ya Dodoma. Anaandika Dany Tibason, Dodoma … (endelea).

Hayo yalielezwa na Ofisa Habari wa mamlaka hiyo, Angela Msimbila alipozungumza na alipozungumza na mwandishi wa habari hii mjini Dodoma leo juu ya mikakati na malengo ya uboreshaji wa Mji wa Dodoma sambamba na ulipaji wa fidia kwa wale wanaopisha maeneo yao.

Msimbila amesema, wamefikia hatua hiyo baada ya kukabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa fedha za kulipa fidia katika maeneo ambayo tayari yamekwishapimwa na mamlaka hiyo.

“Ili kuondokana na lawama kwa wakazi wanaopisha maeneo yao ambayo ni mashamba na viwanja, ambavyo vimepimwa na CDA, mamkala imelazimika kulipa fidia kwanza baada ya kufanyika tathimini,” amesema Msimbila.

Amesema kuchelewa kupima na kulipa fidia kulitokana na ukosefu wa fedha, hata hivyo baada ya kukopa fedha hizo kutoka Benki kutasaidia zoezi hilo kuendelea bila ya malalamiko.

Aidha, umoja wa wabunge katika Mkoa wa Dodoma wenye majimbo 10 kwa pamoja wamekubaliana kuwa, wataishinikiza serikali kutunga sheria ambayo italazimisha mkoa huo kuwa na hadhi ya Makao Makuu tofauti na ilivyo sasa.

Wabunge hao kwa pamoja wakichangia katika kikao kilichofanyika mjini hapa kwa lengo la kutaka kujua changamoto mbalimbali zinazoikabili mamlaka hiyo wamesema, ili kuondokana na sintofahamu ni vyema sasa serikali ikatunga sheria hiyo.

Wakichangia wabunge hao wamesema ni wazi kwamba, serikali ina mpango wa kuhamia Dodoma lakini mpango huo hautiliwi mkazo kisheria.

Kwa upande wake Mbunge wa Kibakwe, George Simbachawene (CCM) amesema licha ya serikali kuwa na mpango wa kuhamia Dodoma lakini kasi yake ni ya kusuasua.

Mbunge wa Viti Maalum, Felista Bura (CCM) amesema mpango wa Dodoma kuwa Makao Makuu ni mkakati wa siku nyingi na aliyekuwa mbunge wakati huo Dk. David Malole alipewa kazi ya kupeleka hoja binafsi bungeni lakini hoja hiyo ni kama ilipotelea hewani.

“Hakuna sababu yoyote ya Dodoma kuitwa Makao Makuu wakati hakuna kinachoendelea, sasa umefika wakati wa kuwepo kwa sheria ambayo inaweka wazi utaratibu wa kuhalalisha Dodoma kuwa Makao Makuu,” amesema Bura.

error: Content is protected !!