Saturday , 15 June 2024
Home Gazeti Habari za Siasa CCM yazindua kampeni Z’bar, Dk. Mwinyi amwaga ahadi
Habari za Siasa

CCM yazindua kampeni Z’bar, Dk. Mwinyi amwaga ahadi

Spread the love

DAKTARI Hussein Ali Mwinyi, Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) ametaja mambo atakayotekeleza endapo atafanikiwa kuchaguliwa katika Uchaguzi Mkuu wa tarehe 27 na 28 Oktoba 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar  … (endelea).

Dk. Mwinyi ameeleza hayo leo Jumamosi tarehe 12 Septemba 2020 katika uzinduzi wa kampeni za urais za CCM uliofanyika Uwanja wa Demokrasia-Kibandamaiti mjini Unguja.

Mgombea huyo wa CCM katika nafasi ya urais, amesema kipaumbele chake cha kwanza ni kuenzi Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na kudumisha Muungamo wa Tanganyika na Zanzibar huku akisisitiza kuidumisha sera ya chama chake ya Serikali mbili.

Dk. Mwinyi amesema, endapo atachaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar, Serikali yake itaweka mkazo maalum kwenye uchumi wa bahari, ili kuongeza pato la nchi na maendeleo ya wananchi.

Katika uimarishaji wa uchumi kupitia bahari, Dk. Mwinyi ametaja maeneo ambayo Serikali yake itaweka mkazo, akianza na eneo la uvuvi.

“Sekta ya uvuvi haijafanyiwa kazi vya kutosha, nimeona muhimu tutoe kipaumbele cha pekee katika suala la uvuvi.”

Dk. Hussein Mwinyi, mgombe wa Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM akichukua fomu ya kuwania nafasi hiyo

“Uvuvi wa bahari kuu, bahari ndogo na uzalishaji samaki.Tujenge viwanda vya samaki na masoko ya kuuza samaki pamoja na kujenga magati madogo ya wavuvi,” amesema Dk. Mwinyi.

Eneo lingine ni uchimbaji na utafutaji wa mafuta na gesi baharini, kwa kuhakikisha mikataba ya ubia kati ya Serikali na wawekezaji kwenye sekta hiyo inawanufaisha wananchi wa Zanzibar.

“Ndani ya uchumi wa blue, kuna eneo la mafuta na gesi tutahakikisha mikataba tunayoingia itakua mizuri yenye kunufaisha wananchi wa Zanzibar. Tutahakikisha kazi zinazoweza kufanywa na Wazanzibar katika utafutaji gesi zinafanywa na Wazanzibar na hatubaki watazamaji,” ameahidi Dk. Mwinyi.

Hali kadhalika katika uimarishaji wa uchumi kupitiabahari, Dk. Mwinyi ameahidi kujenga bandari ya kisasa itakayoweza kukidhi mahitaji ya Zanzibar, ikiwemo kupokea makontena ya mafuta, meli za kitalii na mizigo ya uvuvi, ili Wazanzibar wapate ajira na uchumi wa visiwa hivyo ukue.

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Dk. Hussein Mwinyi akirejesha fomu za kuwania Urais wa Zanzibar ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)

Dk. Mwinyi amesema kipaumbele chake kingine akifanikiwa kuwa Rais wa Zanzibar atalivalia njuga suala la ujenzi wa vyanzo vya uzalishaji umeme, ili wananchi wapate nishati hiyo kwa gharama nafuu na upatikanaji wake uwe wa uhakika.

Mgombea huyo wa CCM ameahidi kuboresha miundombinu ya barabara kwa kujenga barabara za lami zenye urefu wa Kilomita 198 Unguja na Pemba.

Kuhusu huduma za kijamii, Dk. Mwinyi ameahidi kuboresha sekta ya elimu kwa kutoa elimu bora bila malipo, kuongeza ufaulu wa wanafunzi, kufumua upya mitaala ya elimu ya ufundi ili ikidhi soko la ajira pamoja na kuongeza udahili katika vyuo vya ufundi, vikuu.

Kwenye sekta ya afya, Dk. Mwinyi ameahidi kuimarisha huduma za afya kuanzia ngazi ya msingi hadi rufaa, kuongeza vifaa tiba na dawa sambamba na watumishi wa afya.

Dk. Mwinyi ameahidi kuimarisha sekta ya viwanda kwa kujenga viwana vya kutosha ili kupunguza changamoto ya ukosefu wa ajira na kusambaza huduma ya maji maeneo yote ya mijini na vijijini.

Kwenye sekta ya kilimo, Dk. Mwinyi ameahidi kuwekeza kwenye kilimo cha biashara kitakachoenda sambamba na ujenzi wa viwanda vya mazao ya biashara na vyakula yanayozalishwa visiwani humo.

Dk. Mwinyi amesema Serikali yake itapanua wigo wa utalii ili usiwe wa fukwe peke yake bali uwe katika maeneo ya kihistoria na michezo, ili kuongeza idadi ya watalii kufikia zaidi ya 800,000.

“Ili kukuza kwa kasi uchumi wetu tutaweka mkazo maalum kwenye uchumi wa ‘blue’, visiwa hivi vina kila sababu ya kunuifaka na bahari . Tutaongeza nguvu katika kuimarsiha utalii usiwe wa fukwe peke yake bali na mambo mengine ya michezo na maeneo ya historia,” ameahidi Dk. Mwinyi.

Dk. Mwinyi amesema ili vipaumbele vyake hivyo vitekelezwe kikamilifu, ataimarisha utawala bora, umoja na mshikamano.

“Katika eneo la umoja na mshikamano nasema lazima tuujenge tusitoe nafasi kwa ubaguzi wa aina yoyote. Nitaweka utaratibu maalum wa kukutana na wananchi wa chini pamoja na wafanyabaishara na wawekezaji, kwa ajili yakusikiliza changamoto zao na kuzitafutia ufumbuzi,” ameahidi Dk. Mwinyi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

DA, ANC waridhia kuunda serikali ya mseto Afrika Kusini

Spread the loveChama tawala nchini Afrika Kusini cha African National Congress, ANC,...

BiasharaHabari MchanganyikoHabari za Siasa

Mataifa Afrika Mashariki yawasilisha bajeti 2024/2025 inayolenga kukuza uchumi

Spread the loveMataifa manne ya Afrika Mashariki jana Alhamisi yamewasilisha bungeni bajeti...

Habari za SiasaTangulizi

Gesi asilia, petroli kodi juu

Spread the loveWaziri wa Fedha, Dk. Mwigulu Nchemba amependekeza kufanya marekebisho kwenye...

Habari za SiasaTangulizi

Bilioni 155.4 kugharamia kicheko cha wastaafu 2022-2030

Spread the loveWaziri wa Fedha, Dk. Mwigulu Nchemba amesema jumla ya Sh...

error: Content is protected !!