May 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

CCM yawanyooshea kidole Polepole, Askofu Gwajima “subirini matokeo”

Askofu Josephat Gwajima

Spread the love

 

CHAMA tawala nchini Tanzania- Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema, kimeanza taratibu za kuwachukulia hatua makada wake wanaokwenda kinyume na misimamo ya chama hicho. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Ni baada ya wanachama hao wakiwemo wabunge wake wawili, Humphrey Polepole wa kuteuliwa na Askofu Joseph Gwajima wa Kawe kuwa na mawazo yanayokidhana na chama hicho kuhusu chanjo ya corona.

Polepole na Gwajima ambaye ni Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima wamekuwa wakisema hawatachanjwa msimamo unaotofautiana na wa Rais Samia Suluhu Hassan ambaye ni Mwenyekiti wa CCM.

Rais Samia aliwaomba Watanzania wachanjwe chanjo hiyo, kwa kuwa ni salama kiafya na itawasaidia kujikinga dhidi ya UVIKO-19.

Leo Jumatano tarehe 11 Agosti 2021, Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo akizungumza na waandishi wa habari, ofisi ndogo za chama hicho Lumumba, jijini Dar es Salaam, ameulizwa kuhusu mkanganyiko huo.

Humphrey Polepole, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM

Chongolo aliulizwa ni hatua gani zimechukuliwa dhidi ya makada wake wanaotoa misimamo kidhani naya chama akiwemo Rais Samia.

“Kuhusu kauli kinzani dhidi ya msimamo wa chama na Serikali, niseme chama ni kikubwa kuliko mtu yeyote, hata mimi nimepewa dhamana tu. Sina mamlaka ya kuweka ya kwangu na kubeba ajenda zangu.”

“Hao unaofikiria kwamba wanaweza kushindana au kujaribu chama, chama hiki kina utaratibu na tayari taratibu zimeanza, subiria matokeo,” amesema Chongolo.

Katibu Mkuu huyo wa CCM, amesema chama hicho kimeweka utaratibu wa kuwawajibisha wanachama wake wanaokwenda kinyume na misimamo yake na Serikali.

“Chama hiki kimeweka utaratibu wa kuhangaika na mimi nikianza kufanya mambo yangu ya hovyo. Sasa sijui kwenye chama hiki leo hii baada ya mwenyekiti na makamo anayefuata kwa ukubwa ni nani? ni mimi,” amesema Chongolo na kuongeza:

“Sasa kama mimi nina fursa ya kuchukuliwa hatua, nani mkubwa zaidi? Kwa hiyo mtu asifikirie kuna mtu anaweza kuota mapembe, zikawa ndefu kuliko waliowahi kuota nyuma na ninyi mnajua historia,” amesema Chongolo

“CCM imekuwa ikichukua hatua katika mazingira ambayo kila mmoja anapanua mdomo na kushangaa.”

error: Content is protected !!