March 8, 2021

Uhuru hauna Mipaka

CCM yatuhumiwa kuihujumu ilani yake

Bunge la Jamhuri ya Muungano la Tanzania

Spread the love

CHAMA cha Mapinduzi (CCM) kimetuhumiwa kuhujumu ilani yake ya uchaguzi wa mwaka 2015 na wabunge wa upinzani. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Wakizungumza katika nyakati tofauti leo tarehe 14 Novemba 2018 bungeni jijini Dodoma, Mbunge wa Ndanda, Cecil Mwambe na wa Momba, David Silinde wamesema serikali ya CCM imeshindwa kutekeleza baadhi ya ahadi zilizomo katika ilani yake.

Mwambe ameeleza kuwa, katika ilani ya CCM kuna baadhi ya ahadi utekelezaji wake unasua sua, ikiwemo utekelezaji wa baadhi ya miradi ya barabara katika jimbo lake, ambayo CCM iliahidi kutekeleza katika ilani yake.

“Nataka kufahamu kutoka kwa waziri hata ukisoma ilani ya CCM kuna maeneo utekelezaji wake unasua, barabara ya Masasi, Nachingwea, Luhangwa, lini barabara hii itatengenezwa kwa kiwango cha lami kadiri ya ilani ya mapinduzi,” amesema Mwambe.

Akijibu swlai la Mwambe, Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Elias Kuandikwa, amempongeza Mwambe kw akusoma na kuijua Ilani ya CCM, na kusema kwamba serikali imelitazama kwa macho mawili suala la ujenzi wa barabara hiyo, na kwamba iko kwenye hatua nzuri ya kuanza ujenzi.

Kwa upande wake Silinde amesema kuwa, serikali ya CCM imeshindwa kutekeleza ilani yake kutokana na kutodhibiti bei ya baadhi ya pembejeo ikiwemo mbolea, jambo ambalo ni kinyume na ilani hiyo inayoonyesha kwamba serikali ina lengo la kuongeza fedha za ruzuku kwa wakulima ili kuwaondolea mzigo wa pembejeo.

“Pamoja na majibu ya serikali, moja ya jitihada za serikali ni kufuta tozo nyingi na ununuzi wa mbolea kwa pamoja. Ukipitia kwenye ilani ya CCM inaonyesha kwamba walikuwa wana lengo la kuongeza fedha za ruzuku kwa wakulima, pamoja na ilani ya CCM kuzungumza, kwa nini serikali inashindwa kutekeleza ilani yake yenyewe sababu bei ya mbolea inaongezeka,” amesema Silinde.

Akijibu swali la Silinde, Naibu Waziri wa Kilimo na Mifugo, Omary Mgumba ilani ni muongozo wa serikali na hivyo haiwezi kuacha kuitekeleza.

“Kwamba kwa nini serikali ya CCM hatutekelezi ilani ya CCM, kwanza nikupongeze kwa kusoma ilani kujua mambo mazuri yaliyopo, na sisi serikali ilani ni muongozo wetu tunaitekeleza, na ndio maana tukaunda ununuzi wa mbolea wa pamoja ni utekelezaji wa ilani, baada ya kubaini baadhi ya watu wanatia mfukoni fedha za ruzuku ya pembejeo kwa kutumia vocha,” amesema Mgumba.

error: Content is protected !!