Tuesday , 23 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa CCM yateua wagombea uwakilishi Z’bar
Habari za Siasa

CCM yateua wagombea uwakilishi Z’bar

Spread the love

KAMATI Kuu Chama Cha Mapinduzi (CCM) imefanya uteuzi wa wagombea Uwakilishi katika Baraza la Wawakilish (BLW) Zanizbar katika majimbo 50 kwa kuzingatia uwezo, umahiri na utendaji wao. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea)

Kikao cha kamati kuu kimefanyika leo Jumatatu tarehe 31 Aagosti 2020 jijini Dodoma chini ya Mwenyekiti wa CCM, Rais John Magufuli.

Mara baada ya kumalizika kwa kikao hicho, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Humphrey Polepole ameweka bayana kwamba wamejadili, wametafakari, na kuangalia uhodari na ubingwa wa wagombea wa Baraza la Wawakilishi (BLW) ili kuivusha Zanzibar.

Amewataja walioteuliwa kugombea uwakilishi ni Zawadi Amour Nassoro (Konde), Shenata Shaane Khamis (Micheweni), Said Saleh Salim (Tumbe), Tumu Mwalim Masoud (Wingwi), Mariam Dhai Juma (Gando), Makame Said Juma (Kojani), Othman Ali Khamis (Mtambwe), Khamis Dadi Khamis (Pandani), Harous Said Suleiman (Wete), Nadir Abdulatif Yusuph (Chanani) na Juma Makungu Juma (Kijini).

Wengine ni; Abdallah Abbas Wadi (Nungwi), Sulubu Kidongo Amour (Mkwajuni), Haji Omar Kheri (Tumbatu), Mtumwa Bee Yusuph (Bumbwini), Ali Salum Mohamed (Donge), Asha Abdallah Mussa (Mahonda), Shaibu Hassan Kadiara (Chakechake), Suleiman Masoud Makame (Chonga) na Masoud Ali Mohamed (Ole).

Pia wamo; Bakari Ahmad Bakari (Wawi), Suleiman Makame Ally (Ziwani), Bahati Khamis Kombo (Chambani), Mussa Foum Mussa (Kiwani), Abdallah Hussein Kombo (Mkoani), Mohamed Mganza Jecha (Mtambile), Issa Haji Ussi (Chwaka), Simai Mohamed Said (Tunguu), Haji Shaaban Waziri (Uzini), Haroun Ali Suleiman (Makunduchi), Dk. Sudi Dou Hassan (Paje) na Mwanaasha Hamis Juma (Dimani).

Wengine ni; Yusuph Hassan Idd (Fuoni), Suleiman Khamis Suleiman (KiembeSamaki), Ameir Abdallah Ameir (Mwanakwerekwe), Ally Suleiman Ameir (Pangawe),

Pia, kamati kuu imeteua wabunge wa viti maalumu; Shadiz Mohamed Suleimani, Zuhura Mgeni Othumani na Zainabu Omari Amiri ( Mkoa Kusini Pemba), Salma Mussa Bilal, Rahma Kassim Ally na Arafa Ally Yusufu (Mkoa Kusini Unguja), Fatma Ramadhani Mandoba, Mwanaidi Kassim Mussa na Fatma Ally Ameir ( Mkoa Magharibi).

Wengine ni; Saada Ramadhani Mwendwa, Mgeni Hassan Juma na Salma Abdi Ibade (Mkoa Mjini), Mwantatu Mbaraka Hamisi na Zainab Abdallah Salum (Wenye Ulemavu), Riziki Pembe Juma( Wasomi), Salha Mohamed Mwinjuma na Udhaima Mbaraka Tahir (Wawakilishi wa Vijana) na Sabiha Filifili Tani (Wazazi)

Polepole amesema, wagombea hao wameteuliwa kuwania nafasi za uwakilishi kutokana na uwezo wao wa kuchangia katika kuleta maendeleo ya Zanzibar pamoja na mstakabali wa sasa na baadaye kwamba utakuwa katika mikono salama.

Humphrey Polepole, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM

Amesema uamuzi wa kuwateua, umezingatia uwakilishi wa kimakundi rika, mazingira ya Zanzibar, maisha ya leo na kuangalia watu wanaoweza kuleta mawazo mazuri kuhakikisha Zanzibar kama sehemu ya Muungano Baraza La Wawakilishi (BLW) linapata wawakilishi ambao wanasadifu maono ya CCM, Mgombea wa urais wa Tanzania, Rais John Magufuli na mgombea wa Zanzibar, Dk Husseini Mwinyi.

“Tumeshajipambanua kwamba suala la maendeleo kule Zanzibar si mjadala, mwendokasi wa watu wa Zanzibar halina mjadali, tumefanya utafiti mkubwa na kujiridhisha Wazanzibar wanataka ule muziki wa Magufuli wa Muungano pia uakisiwe Zanzibar.”

“Tumepata mtu mpole, mnyenyekevu wa hali ya juu, amehudumu kama kiongozi mwandamizi katika Serikali ya Muungano na Zanzibar,” amesema Polepole.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Serikali kuanzisha mradi wa Gridi ya maji ya Taifa

Spread the loveWaziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema katika mwaka wa fedha...

Habari za Siasa

Rais Samia aridhishwa utendaji mabalozi, awapa neno

Spread the loveRais wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan amewapongeza mabalozi  wanaowakilisha ...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

NMB yadhamini Mkutano Mkuu ALAT, kufunguliwa na Samia

Spread the loveBENKI ya NMB, imekabidhi hundi yenye thamani ya Sh. 120...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mipango na uwekezaji kutumia bilioni 121.3, mradi wa Bagamoyo wapewa kipaumbele

Spread the loveWIZARA ya Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, imeliomba Bunge...

error: Content is protected !!