April 14, 2021

Uhuru hauna Mipaka

CCM yateua mgombea Jimbo la Nasari

John Pallangyo ameteuliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) mgombea wa Ubunge jimbo la Arumelu Mashariki

Spread the love

JOHN Pallangyo ameteuliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM), kugombea ubunge katika Jimbo la Arumeru Mashariki lililokuwa likisimamiwa na Joshua Nasari wa Chadema. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole, Pallangyo ameteuliwa leo tarehe 15 Aprili 2019 na Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC) iliyoketi jijini Dodoma.

Pallangyo kupitia tiketi ya CCM anatarajiwa kugombea ubunge katika jimbo hilo baada ya Nasari kutenguliwa ubunge wake na Ofisi ya Bunge.

Halmashauri hiyo iliyoongozwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais John Magufuli, pia imefanya uteuzi wa wajumbe wanaogombea ujumbe wa NEC kupiti Umoja wa Vijana wa chama hicho (UVCCM) kundi la bara.

Wajumbe walioteuliwa kugombea ujumbe wa NEC ni pamoja na Sara Joel Sompo, Japhary Kabecha Mghamba na Ngusa Charles Juda.

error: Content is protected !!